Facebook

Monday, 12 May 2014

Haiwezekani Bunge kuwa sehemu ya kuficha wezi..

Nimejitokeza kuweka makala hii kimsingi tujadili mambo ya nayoendelea mjengoni, sasa tujadili jambo lililo ibuliwa jana na ndg kafulila,juu ya utafunwaji wa zaidi ya bilioni 200 benki kuu, ni ukweli usiofichika kwa sasa ugonjwa unaolitafuna taifa ili ni ufisadi, unaoratibiwa na baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi, na sema haya kwa sababu zifuatazo,wote tulishuhudia, bwana luhanga mpina, akijaribu kuzima hoja ya bw Kafulila, akisaidiwa na spika Anne Makinda.

Sote ni mashaidi kwamba mambo haya ya zima zima hayakuanza leo, nakumbuka dk wilbod slaa alipoibua tuuma za EPA bungeni, spika wa kipindi kile bw samweli 6 alitishia kumchukulia hatua za nizamu Dk Slaa, kwa kuongea uongo bungeni, mwishowe ikaja kuthibitika ni ukweli fedha zilichotwa kwenye akaunti ya EPA, likaja la richmond demo ikawa ihi ihi mwishowe ukweli ukathibitika, sasa kunataarifa za CAG na takukuru kupewa kazi ya kuchunguza jambo hili.

Ukweli ni kwamba CAG na takukuru katika tuhuma zilizopiti wali wasafisha EPA na Richmond kabla ya kuja kamati teule ya bunge na ripoti ya wizi hambao CAG na TAKUKURU uliubariki.

Kimsingi hapa zitakuja ripoti za safisha safisha kubariki wizi uhu wa fedha ambazo zingetumika kununulia madawati na madawa hospitalini.

Wito wangu kwa viongozi wa chama cha mapinduzi siku zao za kubakia madarakani zinaesabika, na yote walio yafanya wakiwa madarakani na kulindana watawajibika, waliotenda mema watapata thawabu yao

0 comments:

Post a Comment