Orodha ya wasanii watakaoshiriki kwenye Kili Music Tour 2014 imetangazwa leo. Baadhi ya wasanii watakaokuwepo kwenye ziara hiyo wakiwe kwenye picha ya pamoja Mwaka huu zaidi ya wasanii 30 watashiriki katika ziara hiyo kwenye mikoa zaidi ya 10 nchini na itakayoanza ambao Mei hadi Septemba 2014. Wasanii hao ni pamoja na Diamond, Ommy Dimpoz, Linex, Proffesor Jay, Izzo Biznes, Kala
Jeremiah, Fid Q, Snura, Weusi, Ben Pol, Mzee Yusuph, Shilole na Mwasiti. Wengine ni Nay wa Mitego, Mwana FA, Khadija Kopa, Juma Nature, Warriors From the East, Madee, Young Killer, Jambo Squad, AY, Vanessa Mdee, Mashujaa Band, Rich Mavoko na Christian Bella.
Hata hivyo Lady Jaydee aliyekuwepo kwenye ziara hiyo mwaka jana, ameondolewa mwaka huu kwa kile chanzo kimoja kimesema ni kutokana na tweet ya dharau aliyoiandika Lady Jaydee kuhusu kutokufahamu kama tuzo hizo zilifanyika.
Chanzo hicho kimesema pia kuwa Roma alikuwa awepo kwenye ziara hiyo lakini ‘ujuaje wake
umemfanya apigwe chini’.
0 comments:
Post a Comment