Facebook

Thursday 22 May 2014

Mtoto wa 50 Cent alieamua kumchana baba kwa kutotokea kwenye graduation yake



Screen Shot 2014-05-21 at 8.24.48 AM 

Japo ni mara nyingi watoto wa kiume wameonekana kuwa na mapenzi zaidi kwa mama zao kuliko baba, haimaanishi kwamba hawamuhitaji baba kabisa kwenye maisha yao.
Mtoto wa 50 Cent aitwae Marquise Jackson alitegemea baba yake ambae ni 50 Cent angehudhuria graduation yake akiambatana na watu wengine wa karibu na familia ila haikua hivyo.
50 Cent hakutokea ndio maana mwanae huyu alipata hasira mpaka kuzionyesha kwenye mtandao wa kijamii kwa kusema ‘nilitarajia kumuona baba yangu kwenye graduation yangu leo ila hajatokea, mama yangu na dada yangu siku zote wako na mimi… hata hivyo nimefanikisha bila wewe’
Screen Shot 2014-05-21 at 8.18.49 AM

Screen Shot 2014-05-21 at 8.19.11 AM 
Hata hivyo baadhi ya wanafamilia wa Marquise wanasema hii post sio ya ukweli lakini wakati huohuo wengine wanasema imeandikwa na Marquise mwenyewe.
Baadae taarifa zilitoka kwamba 50 Cent anasema hakupewa taarifa siku ya graduation ni lini na vilevile nyingine zinasema alikatazwa kuhudhuria na Mama Marquise.
50 Cent asubuhi ya May 21 2014 kwenye instagram yake zimepatikana picha mbili ambazo zinaonekana zina maneno yanayohusu hii ishu yake na mtoto.
Screen Shot 2014-05-21 at 8.37.03 AM
Screen Shot 2014-05-21 at 8.37.31 AM 

 Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata habari mbalimbali kama hizi na kupata habari kama hizi natakazokuwa nakutumia facaebook kwa ku-like page yetu ya facebook...Bofya hapa uweze ku-like katemimethsela.blogspot.com/facebook

0 comments:

Post a Comment