Mchezaji mmoja wa timu ya ligi ya American Football
(National Footbal League), Michael Sam amekuwa mchezaji wa kwanza wa
mpira wa miguu kutangaza kuwa anajihusisha na tabia za ushoga.
Sam alikuwa ameteuliwa na timu ya Saint Louis Rams katika siku ya
mwisho ya usakaji wa vipaji katika mchezo huo ulio maarufu zaidi nchini
marekani.
Hatua hiyo ya Michael Sam kutangaza jinsia yake mnamo mwezi february
baada ya kukamilisha masomo yake ya mchezo huo katika chuo cha Missouri
ilipongezwa ,huku rais Obama akiwa miongoni mwa watu waliotoa pongezi
zao.
Baadhi ya wachambuzi wa michezo walikuwa wamebashiri kwamba baadhi ya
timu huenda zikajitenga na umaarufu unaomzunguka mchezaji huyo.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment