Muda
mchache baada ya kutangazwa kuwa kocha msaidizi wa klabu ya Manchester
United, mwanasoka Ryan Giggs ametangaza rasmi kustaafu soka.
Giggs ambaye alianza kuichezea timu ya watoto ya Manchester United
mnamo mwaka 1991, amestaafu soka baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa
miaka 23 mpaka sasa huku akifanikiwa kuwa mchezaji aliyecheza mechi
nyingi zaidi katika klabu yake ya Manchester United – akiichezea mara 963.
Giggs anastaafu akiwa ndio mwanasoka
ambaye kashinda makombe mengi zaidi – makombe 13 ya premier league, FA
Cup 4, Capital One 4, mawili ya kombe la klabu bingwa ya ulaya na 2
klabu bingwa ya dunia.
Giggs
pia ameshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa ligi mara mbili mwaka
1992 na 1993, pia alishinda tuzo hiyo kutoka kwa klabu ya Manchester
United mwaka 1991 na 1992.
Mnamo
mwaka 2009 alishinda tuzo ya BBC Sports Personality of the Year na paia
akashinda PFA Player of the Year award. Ametajwa kuwa mchezaji bora
mwaka wa ligi kwa mara 6.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata taarifa mbalimbali za usajili kwa muda muaaka
0 comments:
Post a Comment