Facebook

Wednesday, 21 May 2014

Wazalendo na Wasema Ukweli Tanzania Wanapopukutishwa Bila Woga!!

Hivi inaweza kuwa kweli? Ukimjumlisha na huyu bwana wa EWURA Wazalendo na Wasema Kweli Wataisha.

Kifo cha Mgimwa kiliingia kwenye mlolongo
wa vifo kadhaa vyenye utata vilivyowahi
kutokea nchini katika kipindi cha miaka 20
iliyopita.
Mawaziri wawili waliopata kuongoza Wizara
ya Fedha nao wanadaiwa kufa katika
mazingira ya kutatanisha, miongoni mwao
akiwa Profesa Kighoma Ally Malima aliyekufa
Julai 16, 1995.
Alipojiengua CCM na kuhamia NAREA (NRA),
Prof Kighoma alikwenda Makka katika Hijja
ya UMRA. Kabla ya kwenda kwake huko
aliahidi pindi atakaporudi Tanzania atakuja
kutoa yaliyopo moyoni mwake. Baada ya
kumaliza Hijja alielekea Uingereza na mauti
yakamkuta huko.
Ilienea katika kila kona ya Tanzania kuwa
inawezekana kuna FITNA iliyosababisha kifo
chake japokuwa wengine wanasema hakuna
FITNA yoyote.
Steven Kibona, aliyepata kuwa Waziri wa
Fedha enzi za Alhaj Ali Hassan Mwinyi,
pamoja na aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu,
Gilman Rutihinda, nao walikufa vifo vya
utata.
Kuna taarifa zilizodai kwamba, wazalendo
hao walikataa kuchapisha fedha na
kuziingiza kwenye mfumo kwa kutambua
kwamba kufanya hivyo kungeongeza
mfumuko wa bei na ugumu wa maisha
ungeongezeka.
Kibona alipelekwa na aliporejea huko
akaanza kuumwa. Ikaelezwa kwamba
amekula vyakula vya Kihindi ndiyo maana
alikumbwa na tumbo la kuhara kwa sababu
ya ugeni wa chakula. Hakukaa muda mrefu
akafariki dunia.
Rutihinda naye alipata ajali asubuhi tu akiwa
anatoka nyumbani kwake. Taarifa
zilizokuwepo ni kwamba ilikuwa ajali ya
kawaida!
Mwingine ambaye kifo chake kina utata ni
Horace Kolimba. Huyu anajulikana kwa kauli
yake aliyoitoa kwamba CCM haikuwa na dira
wala mwelekeo. Akaitwa Dodoma 'kuhojiwa'.
Lakini Machi 15, 1997 majira ya saa 11 jioni
wakati akijiandaa kutoa maelezo yake,
akadondoka ghafla. Walipompeleka hospitali
ya Mkoa wa Dodoma tayari alikuwa 'wa
jana'.
Hivi, hakuna anayeweza kutoa taarifa rasmi
kuhusiana na vifo hivi vyenye utata au kifo
cha kiongozi yeyote kinapotokea mpaka
tusubiri 'redio mbao'?
Nawasilisha.
 
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kusoma makala mbalimbali zenazoelezea na kuakisi maisha halisi 

0 comments:

Post a Comment