Mkurugenzi wa wa Vyama na Masuala ya
Kisheria katika Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), Evodius Mtawala, amelazimika kuachia
ngazi kutokana na sababu mbalimbali.
Taarifa ambazo tumezipata, zinaeleza kuwa
Mtawala ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu
wa Simba, alikuwa na hali ya kutokuelewana
na uongozi wa shirikisho hilo na ndiyo
chanzo kikubwa cha kumfanya ang'atuke TFF.
Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa,
alithibitisha kuachia ngazi kwa Mtawala lakini
akasema ni kutokana na sababu mbalimbali
za taaluma yake ya uanasheria.
“Ni kweli Mtawala hataendelea kufanya kazi
TFF lakini ameamua kuchia ngazi mwenyewe
kutokana na sababu mbalimbali alizodai
kwamba ni kujikita na taaluma yake zaidi kwa
sasa, lakini mambo mengine juu ya hilo
yatabaki kuwa siri baina yake na mwajiri
wake.
“Ila mpaka makubaliano ya mwisho yalieleza
kuwa itakapofika mwisho wa mwezi wa nane
(jana 31, Agosti) atakuwa tayari
ameshakabidhi ofisi na kuendelea na masuala
ambayo alidai anahitaji kujikita zaidi
kulingana na taaluma yake,” alisema
Mwesigwa.
Mtawala amedumu kwenye wadhifa huo kwa
miezi nane tu tangu alipoteuliwa Desemba
24, mwaka jana chini ya uongozi wa rais
mpya, Jamal Malinzi
Monday, 1 September 2014
Baada ya "Magumashi" Evodius Mtawala aachia ngazi TFF
Related Posts:
Simba yazinduka taifa na kushusha kipigo kizito kwa Prisons. Wekundu wa Msimbazi Simba SC imefanikiwa kurejesha heshima na kutuliza nyoyo za mashabiki wake baada ya kuitungua Tanzania Prisons jumla ya mabao 5-0 katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa katika dimba la taifa jijini … Read More
Majeruhi yazidi kumuandama Jack Wilshare,afanyiwa upasuaji tena. Kiungo wa klabu ya Arsenal "The Gunners" Jackei Wilshere (23) amefanyiwa upasuaji ikiwa ni tiba ya kutibu maumivu ya kifundo cha mguu wake wa kushoto . Akizungumza na waandishi wa habari, Kocha wa Arsenal Arsene Wen… Read More
BantuTZ LIVESTREAMING:-Angalia mechi zote kali za leo ligi mbalimbali barani Ulaya Katika SIMU,TABLET au COMPUTER yako. Kwa mara nyingine tena kupitia BantuTz LiveStreaming utaangalia Mechi zote za leo Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.'LiveStreaming' kupitia Simu,Computer au Tablet yako. Utaangalia mechi hizo bila kukwama au kukatika kwa… Read More
BantuTz MAGAZETINI:-SOMA KILICHOANDIKWA KATIKA MAGAZETI YOTE YA LEO MACHI 1BantuTz MAGAZETINI:Ni miongoni mwa huduma bora kabisa tunazozitoa ili wewe mdau wa Bantu usipitwe na habari,stori au taarifa yoyote ile.Tunakuletea kila tunachokipata kwa wakati na muda muafaka.Soma kilichoandikwa katika ku… Read More
Rooney aing'arisha Manchester United. Mkwaju wa penalti uliofungwa na nahodha Wayne Rooney uliisaidia Manchester United kuichapa Sunderland mabao 2-0 baada ya West Brown kupewa kadi nyekundu katika kile kilichoonekana kama maonevu. Rooney alifunga baa… Read More
0 comments:
Post a Comment