Facebook

Monday, 1 September 2014

Falcao akubali kutua Manchester United kwa mkopo wa Muda mrefu.

Taarifa tulioipata BantuTz SPORTS hivi punde ni kwamba mshambuliaji hatari kutoka Klabu ya AS Monaco ya Ufaransa amekubali kujiunga na Manchester United kwa mkopo wa Muda mrefu huku akiwa anapokea mshahara unaokadiriwa kuwa Paundi laki mbili [£200000/=] za kiingereza.

Falcao alipita katika klabu mbalimbali zikiwemo FC Porto,Atletico Madrid na alikuwa klabu ya As Monaco ya Ufaransa kabla ya kuhama leo hii na kwenda kujiunga na Mashetani Wekundu.

REKODI YA UFUNGAJI YA RADAMEL FALCAO.

17 matches sub1 11goals AS Monaco

LIGI KUU

67 matches sub1 52goals Atletico Madrid.

48 matches sub3 41goals FC Porto

73 matches sub18 34goals River Plate

MASHINDANO MENGINE

16matches sub2 16goals Monaco

21matches sub1 21goals ATM

Jumla katika ligi nyingine 37matches sub3 Magoli 37

Jumla ya yote mechi 205 sub 25 Magoli 138 .

Manchester United waliokatika kipindi kugumu tangia msimu uliopita wanamchukua Falcao atakaeziba mianya katika timu hiyo hasa kutokana na kuondoka kwa Javier Hernandez Chicharito aliyejiunga Real Madrid kwa mkopo na Muingereza Danny Welbeck atakayejiunga na Tottenham Hotspurs au Everton ambazo zimeambiwa zitoe kitita cha Paundi Milioni 5 kuweza kumpata mshambuliaji huyo kwa Mkopo.

Radamel Falcao anatarajiwa kupanda ndege binafsi mida ya saa 9 Alasiri kutoka Nice-Ufaransa na kuelekea katika Jiji la Manchester kufanyiwa vipimo na hatimaye kujiunga rasma na timu hiyo.

Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze kupata kila taarifa ya usajili katika siku hii ya leo ambapo majira ya saa 8 usiku kwa Masaa ya Afrika Mashariki dirisha hilo linatarajiwa kufungwa.

Related Posts:

  • Tetesi za usajili katika magazeti mbalimbali barani Ulaya.           Kiungo wa Juventus Arturo Vidal ameipa pigo Manchester United kwa kudai hatokwenda Old Trafford (Daily Mail),    Liverpool watatumia madai hayo kumfuatilia kwa makini Vi… Read More
  • Drogba arudi Chelsea.      Mshambuliaji wa Ivory Coast Didier Drogba amesaini mkataba wa mwaka mmoja kujiunga tena na Chelsea. Drogba, 36, alishinda makombe 10 akiwa na Chelsea kuanzia mwaka 2004 hadi 2012, na alikuwa mchezaji… Read More
  • Vidal "Siendi Manchester United"   Arturo Vidal amesisitiza kuwa haendi Manchester United msimu huu. Mchezaji huyo kutoka Chile amekuwa akihusishwa na kuhamia Old Trafford kutoka Juventus, Man United wakiwa tayari kuvunja rekodi yao ya uhamisho.… Read More
  • Nigeria kuzungumza na Stephen Keshi NFF inajadiliana na Keshi kuhusu kandarasi mpya Shirikisho la kandanda la Nigeria NFF limesema kuwa linaanda mikakati ya kufanya mazun… Read More
  • Lampard ajiunga rasmi na New York City FC.   Frank Lampard amekamilisha uhamisho kujiunga na klabu ya ligi ya Marekani - MLS ya New York City FC baada ya kutambulishwa hii leo. Frank sasa ana miaka 36 na ameiwakilisha Chelsea kwa misimu 13 na kufunga bao 211 … Read More

0 comments:

Post a Comment