Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anataka
kununua mshambuliaji mpya kabla ya dirisha
la usajili kufungwa Jumatatu.
Huku mshambuliaji wao Olivier Giroud akiwa
majeruhi, Arsenal walilazimishwa sare ya 1-1
na Leicester iliyopanda daraja, katika mchezo
wa siku ya Jumapili, licha ya kupiga mikwaju
24 iliyolenga goli.
Baada ya mchezo huo, Wenger aliulizwa
kuhusu safu yake ya ushambuliaji na alisema:
"Tuko macho katika dirisha hili la usajili.
Tunafanya kazi kwa nguvu kutafuta suluhu.
"Hakuna anayeweza kubashiri kitakachotokea
katika saa 24 zijazo."
Giroud, ambaye alifunga mabao 16 ya Ligi
Kuu msimu uliopita, amefunga magoli mawili
msimu huu, na aliumia katika mchezo dhidi
ya Everton wiki ikiyopita. Giroud hatocheza
hadi mwishoni mwa Disemba, baada ya
kufanyiwa upasuaji katika mguu alioumia.
Monday, 1 September 2014
WENGER "YUKO MACHO" KUTAFUTA MSHAMBULIAJI
Related Posts:
Moyes mbioni kujiunga Galatasaray. Aliyekuwa kocha wa Manchester United David Moyes ameahidiwa kitita cha pauni milioni £4 kwa mwaka ilikumrithi Roberto Mancini kam… Read More
Barcelona inataka kumsajili Suarez licha ya adhabu kali aliyopewa. Licha ya kukabiliwa na marufuku ya FIFA ya miezi minne kwa kumng'ata mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini Barcelona ya Uhispania haijakata tamaa ya kum… Read More
Manchester United mbion kunasa saini ya kisiki cha Uholanzi,Arsenal na Man Utd zatiana pembe kwa Vidal Karibu vyombo vingi vya habari vimeripoti kuwa Manchester United na klabu ya Feyernood vimefikia makubaliano ya kumsajili beki wa kati Stefan de Vrij kwa thamani ya Paund mil 8.. Beki huyo nguzo kwa timu ya ta… Read More
Manchester United yarusha ndoano kwa Alexis Sanchez Manchester United imetupia macho kwa mchezaji wa Barcelona na Chile,Sanchez £40mil Baadhi ya magazeti nchini Uingereza leo asubuhi na kituo cha SkySport kimezungumzia hili. … Read More
Maximo kuinoa Yanga kwa miaka miwili Kocha mpya wa klabu ya Yanga Maxio Maximo. Maximo alikuwa kocha wa zamani wa timu ya taifa Taifa Stars. Aliyekuwa kocha wa Timu ya Taifa ya hapa nchini Maxio Maximo kutoka Brazil amepata fursa ya kurudi tena hapa n… Read More
0 comments:
Post a Comment