Facebook

Thursday, 1 May 2014

Hasira kwa kukamatwa vijana 9 wanaomiliki Blog huko Ethiopia

Wanablog wa Zone 9

Hatua ya serikali ya Ethiopia kuwakamata wanablog 9 imezua hasira kwenye mitandao ya kijamii.
Wanablog hao maarufu nchini Ethiopia walikamatwa mwishoni mwa wiki huku waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry akitarajiwa kuzuru nchi hiyo.
Mnamo siku ya Ijumaa saa kumi na moja jioni , simu za wanablog 9 zilianza kulia bila kukoma.
Pia walipata ujumbe mwingi tu wa barua pepe
Ujumbe ulikuwa kwamba mmoja wa kikundi cha wanablog tisa, kijulikanacho kama Zone 9 alikuwa amekamatwa, huku wengine wakipata onyo kali.
Lakini inaonekana onyo lilikuja mapema mno. Wanablog wengine watano na wandishi habari watatu pia walikua wamekamatwa.
Wote tisa bado wanazuiliwa huku polisi wakifanya uchunguzi kwamba wanablog hao walikuwa wanashirikiana na mashirika ya kigeni , wanaharakati wa kutetea haki za binadamau na kutumia mitandao ya kijamii kuhatarisha usalama wa nchi.
Bila shaka kukamatwa kwa wanablog hao, kunaonyesha hali ya kisiasa ilivyo nchini humo na jukumu la mitandao ya kijamii katika siasa za nchi.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamekuwa yakilalamika kuhusu ukosefu wa uhuru wa kujieleza nchini Ethiopia.
Vituo vingi vya televisheni na radio vinamilikiwa na serikali.
Kwa sababu ya hali hii nchini Ethiopia , wanaharakati wengi pamoja na wanablog wamekuwa wakitawala mitandao ya kijamii na blog ili kuweza kutoa maoni yao kuhusu kinachoendelea nchini humo na pia kuelezea hasira yao kufuatia kukamatwa kwa wanablog hao.
Wanablog wa Zone 9, waliungana miaka miwili iliyopita na kuanza kutumia mitandao kukosoa serikali wakiituhumu kwa kukiuka haki za binadamu na kujenga miundo msingi duni.
Duru zinasema kuwa msako wa serikali ni jibu lake kwa taarifa ya kundi hilo iliyowekwa kwenye mtandao wa Facebook kuwa wataanza tena harakati zao kwenye blog hiyo baada ya miezi kadhaa ya kusitisha shughuli zao.

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kupata taarifa zilizojiri sehemu mbalimbali za dunia

0 comments:

Post a Comment