Facebook

Thursday, 1 May 2014

Hatimaye msaada wawasili Jamhuri Ya Afrika ya Kati.................



Mamia ya watu wanasubiri kupokea chakula katika kituo kimoja mjini Bangui
Shirika la chakula duniani limesema kuwa ndege inayobeba chakula cha msaada kwa watu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, imewasili mjini Bangui.
Tayari tani 82 za Mchele zimeingizwa nchini humo kutoka nchi jirani ya Cameroon.
Shirika hilo, linatarajia katika mwezi mmoja ujao, kuweza kulisha karibu wakimbizi laki moja na hamsini.
Chakula kingine cha tani 1,800 kitapelekwa nchini humo mwezi ujao.
Hata hivyo, inakadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni moja nchini humo wanahitaji chakula.
Mapigano yameendelea kuchacha katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na kutatiza shughuli ya kuingiza chakula nchini humo kwa kutumia barabara.
Wakati huohuo, walinda amani wamekosa kuzuia mauaji ya waisilamu. Hii ni kwa mujibu wa shirika moja la kutetea haki za binadamu.
Mashambulizi yanayofanywa na wapiganaji wakristo yamesababisha msururu wa waumini wa kiisilamu kutoroka nchini humo kutafuta hifadhi katika nchi jirani.
Mashirika ya misaada yametoa tahadhari ya uhaba wa chakula kutokana na maduka yaliyokuwa yanamilikiwa na wasilamu kufungwa.
Wakati huohuo,Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian, amewasili nchini humo , kama sehemu ya juhudi za kimataifa za kujaribu kumaliza ghasia katika taifa hilo.
Wanajeshi 1600 wa Ufaransa wapo nchini humo kama sehemu ya kikosi cha kimataifa cha kulinda amani.
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon ameiomba serikali ya Ufaransa kuongeza kikosi chake katika Jamhuri ya Afrika ya kati kuzuia kugawanyika kwa taifa hilo na kuwepo maeneo ya waisilamu na wakristo.
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu, Amnesty International linasema walinda amani wa kimataifa wameshindwa kuzuia mauaji hayo.

Related Posts:

  • Mfalme wa Uhispania aachia ngazi Familia ya Carlos imekumbwa na kashfa za ufusadi na uwindaji haramu Mfalme wa Uhispania Juan Carlos anaachia mamlaka, waziri mkuu Mariano Rajoy ametangaza. Juan Carlos, mwenye umri wa miaka 76, amekuwa mfalme tangu … Read More
  • Mwanamke ‘apewa’ daraja la upadri Hilo ni pigo jipya kwa Kanisa Katoliki ambalo kwa siku za karibuni lina kilio cha kutaka mapadri waruhusiwe kuoa huku Papa Francis akieleza msimamo wake kuwa angependa kuendelea kuwa na mapadri waseja Sherehe za upadri… Read More
  • Msichana Mwenye Umri wa Miaka 15 Abakwa kwa Zamu na Wanaume zaidi ya 38 Kuna baadhi ya binadamu wana roho mbaya zaidi ya wanyama wakali wa mwituni na ukisimuliwa matukio waliyofanya unaweza kujiuliza kama kweli ni binadamu au ‘mashetani’! Siku mbili baada ya kuripotiwa habari ya… Read More
  • Wanawake wabakwa gerezani - DRC Wanawake wabakwa gerezani DRC Utafiti uliofanywa na shirika moja la misaada Uingereza umeonyesha kuwa ubakaji unatumiwa tena kwa kiasi kikubwa gerezani kama adhabu kwa wanawake wanaojihusisha na masuala ya siasa … Read More
  • kampeni ya 'Bring Back our Girls' yapigwa marufuku Nigeria Polisi nchini katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja wamepiga marufuku maandamano ya watu wanaowaunga mkono zaidi ya wasichana wa shule mia mbili waliotekwanyara na kundi la wanamgambo wenye itikadi kali za kiislamu la Bo… Read More

0 comments:

Post a Comment