Timu ya Manchester United imeripoti faida ya asilimia 20 katika kipindi cha msimu huu ambao haikunawiri uwanjani .
Katika kipindi cha miezi mitatu ya mwisho wa
msimu huu The Red Devils walisajili faida ya pauni milioni 11
ikilinganishwa pauni milioni 3.6m iliyopata mwaka tangulia.Timu hiyo inasemekana imeandikisha mkataba wa miaka mitatu na kocha wa Uholanzi Louis van Gaal anayetarajiwa kuchukua pahala pa David Moyes,aliyetimuliwa mwisho wa mwezi uliopita kufuatia msururu wa matokeo duni.
Tangazo rasmi litatolewa juma lijalo baada ya Kocha huyo kukamilisha maandalizi ya mechi ya kujipima nguvu dhidi ya timu ya Equador.
Ed Woodward,kaimu mwenyekiti Man Utd
" ''mnajua hatukufanya vyema msimu uliopita na tulimaliza katika nafasi ya 7 nje ya mshindano yeyote ya bara Uropa kwa hivyo hatuna budi kununua wachezaji ilikuimarisha uwezo wa timu yetu katika msimu ujao'."
Mapato kutokana na hati ya upeperushaji wa mechi za timu hiyo yaliimarika kwa asili mia 64 ama pauni milioni 35.6m ilihali faida iliyotokana na uuzaji wa tiketi za mechi ilileta pauni milioni £37.1m.
Kutokana na faida hiyo kubwa Manchester united ilipunguza deni lake kwa takriban pauni milioni 16 na sasa deni lililosalia ni pauni milioni £351.7m.
Kulingana na kampuni ya uhasibu ya Deloitte Football Money League, Manchester United inaorodheshwa ya nne bora miongoni mwa vilabu tajiri zaidi duniani.
Hisa zaklabu hiyo zilianza kuuzwa kwenye soko la hisa la New York Stock Exchange mwaka wa 2012 .
0 comments:
Post a Comment