Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kwamba milipuko miwili imetokea karibu na Soko kubwa la nguo la Gikomba mjini Nairobi.
Watu kadhaa wameripotiwa kujeruhiwa na kuna hofu ya wanne kupoteza maisha yao kufikia sasa.Milipuko ya leo imetokea siku moja baada ya Uingereza kutoa onyo kwa raia wake wanaoishi nchini humo kurejea makwao kwa hofu ya usalama na pia baada ya tahadhari kutolewa ya kutokea kwa mashambulizi ya kigaidi nchini humo.
Gikombaa ni soko kubwa la kuuza nguo ambalo linapakana na mtaa wa Eastleigh ambako wasomali wengi wanaishi na kufanya kazi.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kujua kila kitakachokuwa kinatokea kenye hususan milipuko ya maramara kwa mara inayotokea
0 comments:
Post a Comment