Mwenyekiti wa Manchester City
Khaldoon Al Mubarak amesema kuwa mabingwa hao wapya wa ligi kuu ya
Uingereza wataimarisha kikosi chao licha ya marufuku waliopigwa na
shirikisho la kandanda barani ulaya UEFA kwa kukiuka kanuni za matumizi
ya fedha.
City ilipigwa faini ya pauni milioni £49m, mbali
na kuruhusiwa kuwasajili wachezaji 21 pekee katika msimu huu mpya
kushiriki katika ligi kuu ya mabingwa barani ulaya.Kutokana na faini hiyo ya Uefa Manchester City wameshurutishwa kutotumia mshahara unaozidi ule waliotumia msimu huu katika msimu ujao wa 2014-15 .
Licha ya hayo Mubarak, amesema kuwa wamiliki wa klabu hyo wanafahamu fika matakwa ya UEFA na kuwa watamuunga mkono kwa hali na mali kocha Manuel Pellegrini wakati wa usajili msimu ujao.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 60 kutoka Chile mwaka 2013 baada ya Roberto Mancini kufutwa kazi.
0 comments:
Post a Comment