Watu wengi waliokutana na picha hiyo wameifananisha suruali hiyo na nguo
maarufu kwa akina dada "kipedo" huku wakidai kuwa viatu alivyovaa ni
vya kike.
Omary Nyembo a.k.a Ommy Dimpoz amefunguka ya kwake juu ya madai hayo na kusema....
"Viatu sio vya kike kwasababu, ukisema viatu vya kike it means labda
umeende ku-shop kwenye duka la vitu vya kike, na viatu vile mi nimenunua
South africa, kipindi tumeenda kumsapoti AY kwenye Channel O. Nakumbuka
tena siku ambayo nimeenda ku-shop nilikuwa na Dulla Spatan, nilinunua
kama pea ishirini thelethini, zilikuwa pea nyingi, unajua sometimes
unaweza kuingia kwenye maduka ukakuta kuna sale nini, kwahiyo nilikuta,
galafu na vile vilikuwa ni vyepesi havichukui kilos, kwahiyo nikanunua
nunua vile vingi, lakini nime-shop kwenye Mr Price nakumbuka, vilikuwa
ni simple......"
"sidhani kama watu wameichukuliaje lakini may be labda fashion ndio
imenikosti, lakini naona ni viatu vya kawaida na watu wanavaa, hata
ukiangalia ma designers nini hata watu wengi wanavaa, kwahiyo kwa
kununua mi nimenunua sehem ya vitu vya kiume na hakikua kimoja kusema
labda wamekosea wamekiweka sehem tofauti, ni kwamba viko vingi na design
tofauti...." amesema Ommy
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kupata stori mbalimbali zinazowahusu wasanii
0 comments:
Post a Comment