Kiongozi wa Sinn Fein Gerry Adams amekamatwa
Polisi huko Ireland Kazkazini
wamemkamata mwanasiasa mashuhuri wa chama cha Sinn Fein ,Gerry Adams kwa
kuhusishwa na mauaji yaliyotokea yapata zaidi ya miaka 40 iliyopita.
Adams anahojiwa kuhusu mauaji ya Jean McConville
ambaye alitekwanyara na kundi la waasi la IRA mnamo mwaka 1972 na kisha
akapatikana amepigwa risasi na kuuawa .Kiongozi huyo amekanusha kuhusika kivyovyote vile akisema kuwa alijipeleka binafsi kuzungumza na polisi ilikujaribu kusuluhisha madai hayo yaliyomwandama kwa miaka mingi mno .
Adams anakanusha kuhusika kwa vyovyote vile na utekaji nyara wala mauaji yake bi McConville ambaye alikuwa mama wa watoto kumi .
Adams anazuiliwa kutokana na kifo cha mjane huyo aliyetekwa nyara na kundi la IRA mwaka wa 1972 .
Madai haya yanafwatia mahojiano mjini Belfast mwaka wa 2001-2006 baina ya chuo kikuu cha Boston Marekani na wakereketwa wa vita hivyo vilivyonuiwa kuikomboa Ireland kutoka kwenye minyororo ya ukoloni.
chuo hicho kililazimishwa kutoa sehemu ya mahojiano kwa serikali ya Ireland.
Mmoja kati ya watu 16 waliosemekana kutoweka ni bi McConville .
Mjane huyo alilaumiwa na IRA kuwa mpelelezi wa polisi lakini baada ya ufafanuzi wa polisi yapata mwaka wa 1999, McConville ilibainika kuwa hakuwa.
Kundi hilo la IRA lilikiri kutekeleza mauaji yake bi McConville mwaka wa 1999 lakini mwili wake ulipatikana mwaka wa 2003 ukiwa umetupwa kwenye ufukwe wa bahari.
IRA inashtumiwa kwa kampeini na mauaji yaliyotikisa Ireland kaskazini kwa takriban miaka thelathini.
0 comments:
Post a Comment