Wanaharakati wamepinga vikali kuwaua Nguruwe wakisema ni kinyume na haki za wanyama
Mji wa Shivpur nchini India
umejikuta matatani baada ya maafisa wake kuwataka watu wanaomiliki
bunduki kuwapiga risasi Nguruwe wanaozurura mjini na kuwa kero kwa
wakazi.
Wakazi waliamrishwa kubeba bunduki zao pamoja na
lesene zao kuthibitishwa wana idhini ya kumiliki bunduki ili kuweza
kushiriki zoezi hilo. Taarifa hii ni kwa mujibu wa jarida la Hindustan
Times NewspaperWaliongeza kuwa wale watakaoruhusiwa kuwaua Nguruwe hao watateuliwa mwezi Mei.
Kero la Nguruwe wanaorandaranda mitaani nchini India
‘‘Huu ni unyama na sio suluhu la tatizo la wanyama hao kurandaranda mjini,’’alisema Puneet Tripathi, mwasisi wa shirika la kutetea haki za wanyama na mazingira.
‘‘Lazima maafisa wangalie njia zengine za kusuluhisha tatizo hilo labda kwa kuwahamisha wanyama hao hadi katika mji mwingine,’’ aliongeza bwana Puneet.
Baadhi ya wanaharakati wanasema kuwapiga risasi Nguruwe itakuwa kinyume na sheria za India kuhusu ukatili.
Nguruwe wameonekanakama kero sio mjini humo pekee bali pia katika miji mingine nchini India. Huonekana mara kwa mara wakipekuwa kwenye majaa ya taka wakitafuta chakula.
0 comments:
Post a Comment