Facebook

Friday, 5 September 2014

Boko Haram wazuia watu kuzika maiti


Wapiganaji wa Boko Haram wamesababisha maafa Kaskazini ya Nigeria ngome yao ya vita
Taarifa za kutisha zimeibuka kutoka mjini Bama moja ya miji ambayo ilitekwa na wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram Kaskazini Mashariki ya Nigeria
Seneta mmoja wa eneo hilo,Ahmed Zanna, alisema kwamba wakazi hawaruhusiwi kuwazika jamaa wao waliouawa na wapiganaji hao.
Inaarifiwa miili imetapakaa katika barabara za mji huo ambao Boko Haram imeuteka.
Kundi hilo linasemekana kuuteka mji huo huku wapiganaji wa kundi hilo wakishika doria katika barabara zake.
Maelfu ya watu wametoroka huku idadi kubwa ya wengine wakiuawa.
Seneta huyo ameitaka serikali ya Nigeria kupeleka wanajeshi mjini Maiduguri ambao ni mji mkuu wa jimbo hilo ili kuulinda dhidi ya wapiganaji hao.
Mnamo siku ya Jumatano serikali ya jimbo hilo ilikanusha madai kuwa jimbo hilo limetekwa na wapiganaji hao.
Maafisa wakuu wanakisia kuwa watu 26,000 wameachwa bila makao kutfuatia mapigano katika mji wa Bama.
Bwana Zanna anasema kuwa barabara za mji huo zimejaa miili ya watu na Boko Harama imewakata wakazi kuwazika jamaa wao. ''Kwa hivyo hali ni mbaya na inaendelea kuzorota,'' asema bwana zANNA
Boko Haram wameteka miji kadhaa Kaskazini Mashariki ya Nigeria, katika miezi ya hivi karibuni na kusababisha hofu kuwa huenda wakaufikia mji mkuu Maiduguri.
Bwana Zanna amesema kuwa itakuwa janga kubwa ikiwa Boko Haram wataushambulia mji wa Maidiguri ambao una watu zaidi ya milioni mbili.

Related Posts:

  • Nyama ya Kiboko yawaletea maafa Afrika KusiniWatu kumi walikanyagwa na gari lililokuwa linakwenda kwa mwendo wa kasi walipokuwa wanajaribu kujipatia angalau kipande cha nyama ya Kiboko mwishoni mwa wiki. Taarifa hii ni kwa mujibu wa mtandao wa Daily Nation. Kiboko huyo … Read More
  • Mahakama:Pistorius hakukusudia kuuaJaji anayetoa uamuzi katika kesi ya mauaji inayomkabili Oscar Pistorius, amesema upande wa mashitaka umekosa kuthibitishia kikamilifu shitaka kuu la kwanza dhidi ya Pistorius kuwa alikusudia kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp… Read More
  • Miaka 8 jela kwa jaribio la kutaka kumuua mkosoaji wa Rais wa RwandaWatu wanne - Watanzania wawili na Wanyarwanda wawili- waliokutwa na hatia ya kutaka kumuua mkosoaji wa Rais wa Rwanda Paul Kagame nchini Afrika Kusini wamehukumiwa kwenda jela kwa miaka minane kila mmoja. Mkuu wa zamani wa je… Read More
  • Tahadhari kuhusu gesi za sumuMkuu wa shirika la utabiri wa hali ya anga la Umoja wa Mataifa Michel Jarraud, ametoa tahadharti kuwa dunia nzima inapaswa kushughulikia mabadiliko ya hali ya anga haraka iwezekanavyo la sivyo muda unakwisha. Takwimu mpya kut… Read More
  • Binti alazimisha penzi kwa kumshikia Bastola mwanaume.Marekani: Binti (25) akamatwa kwa kosa la kumlazimisha kijana (33) kufanya naye mapenzi akiwa kamshikia bastoka kwenye gari lake baada ya kijana huyo kuomba lift. Inasemekana huyo binti alikuwa na mwanamke mwingine ambaye wal… Read More

0 comments:

Post a Comment