Facebook

Monday, 19 May 2014

Je unamjua Producer Mtanzania Anaedaiwa Kuwa Mpenzi Mpya wa Nazizi .......Aeleza Jinsi Walivyokutana

Suala la 'nani ni mpenzi mpya wa Nazizi baada ya kuachana na mmewe' lilipata jibu pale ambapo mtayarishaji wa muziki wa Homeboyz records, mtanzania Hery Sappy alipotuma picha zilizojieleza kuwa yeye ndiye.

Hata hivyo, jibu hilo liliingiwa shaka Nazizi alipoulizwa kuhusu hilo; alikanusha na kudai kuwa wao ni marafiki tu na walipiga picha kawaida na kwamba zipo picha nyingi hata zaidi ya hizo.


Nina marafiki wengi wa kiume, tunapiga picha kila mahali. Hivyo ndivyo uhusiano wangu na marafiki zangu ulivyo.” Nazizi aliiambia Nairobi News  March mwaka huu.

Producer Sappy amefunguka kuhusu jinsi walivyokutana na First Lady wa Necessary Noise.


Akiongea na Pulse, Sappy amesema kuwa walikutana October mwaka jana  baada ya Nazizi kufika Homeboyz kukutana na mtayarishaji maarufu ambaye alikuwa anapika hits kadhaa pale.


Ikiwa ni mara ya kwanza kukutana Sappy anaeleza kuwa walizungumza kuhusu kumtayarishia albam nzima na kwamba baada ya hapo hawakukutana hadi February.


"
We met back in October when she came to Homeboyz to meet a famous producer who had been churning out hits. We met and talked about her intentions to have me produce her album. We did not meet again as she was still relocating to Kitengela from Lamu. We hooked up again in February and it has been bliss ever since." Amesema Sappy.

Sappy alikazia wakati anajibu swali kuwa Nazizi ameteka umakini na mizuka yake


Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kupata habari mbalimbali zinazowahusu mastaa bila kwa wakati muafaka bila zengwe 

0 comments:

Post a Comment