Facebook

Thursday, 15 May 2014

Usiombee Kuugua Dengue, Kipimo ni Sh50,000


Wakati taharuki iliyosababishwa na mlipuko wa homa ya dengue ikiendelea kutikisa kila kona ya jiji, imebainika kwamba gharama za vipimo katika hospitali mbalimbali zinafikia Sh50,000, ikiwa ni tofauti kubwa na Sh1,000 kwa kipimo cha malaria.

Ugonjwa huo unazidi kusambaa jijini Dar es salaam na baadhi ya mikoa, kiasi cha mamlaka kuagiza mabasi yote yaendayo mikoani yafanyiwe usafi wa kunyunyizia dawa za kuua wadudu kudhibiti usienee zaidi mikoani. Pia wananchi wameshauriwa kuvaa nguo ndefu ili kudhibiti mbu wanaoeneza ugonjwa huo mchana tofauti na mbu wa malaria

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kupata taarifa mbalimbali 

0 comments:

Post a Comment