Lionel Messi alifunga bao la pekee na la ushindi katika dakika ya mwisho ya mechi baina ya Argentina na Iran ya kundi G.
Mechi hii ilikuwa na kila dalili ya kuishia sare
tasa sawa na ile ya kwanza kati ya Iran na Nigeria ambapo vijana wa
Carlos Queiroz walizima kila dalili ya shambulizi kutoka kwa Argentina.Irana kwa upande wao walikuwa wamedhibiti Nigeria na wakajizolea alama moja kutokana na sare tasa .
Licha ya juhudi zake Jala Hosseini Ashkan Dejagah mechi hiyo ilikuwa imesalia kuwa Argentina wanashambulia nao Iran wakihimili mashambulizi yote.
Argentina licha ya kuwa wamesalia na mechi moja dhidi ya Nigeria sasa wananafasi nzuri ya kuwania kombe la dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 1986.
0 comments:
Post a Comment