Februari ya kila mwaka huenda ikawa ni kumbukumbu mbaya kwa
mwanamitindo na Miss Tanzania 2001, Hapiness Millen Magese ambaye
mwezi huo ndipo alipogundulika kuwa hataweza kupata mtoto
katika maisha yake yote.....
Hali hiyo ndio imemlazimu mwanamitindo huyo kuanzisha taasisi ya
kuwasaidia wanawake wengine hapa nchini ili waepuke kile
ambacho kimemkuta yeye baada ya kuondolewa uzazi kwa ugonjwa
ambao hapendi kusikia unamtokea mwanamke mwingine.....
"Nikiwa sekondari nilikuwa napatwa na ugonjwa ambao kwa wakati
huo niliona ni wa kawaida.Nilikuwa napata maumivu makali wakati
wa hedhi yaliyonisababishia kutapika na wakati mwingine
kupoteza fahamu," anasema.
"Kila nilipoingia kwenye hedhi nililazimika kulazwa kwa siku
sita hadi kumi hospitalini,kutokana na maumivu hayo kuna wakati
wanafunzi wenzangu waliwahi kunihoji ni kwa nini mimi kila
mwezi lazima niugue," anasimulia
Anasema ilifika wakati wakawa wanamhesabia tarehe kutoka siku
anayotoka hospitali hadi mwezi mwingine atakapolazwa tena
"Niliteseka sana, nakumbuka kuna siku nilizidiwa wakati mama
yangu hayupo.Baba akachukua jukumu la kunibeba na kunipeleka
hospitali," anasema.
"Nilipokuwa kwenye maumivu makali aliniambia nijikaze kama
mwanamke, hivyo nikawa namficha baba maradhi yangu, ingawa
ilikuwa kila mwezi kama siyo kunipeleka hospitali yeye basi
lazima aje kunitazama hospitali."
Anasema hata baada ya kujiingiza kwenye masuala ya urembo, bado
hali ya maumivu wakati wa hedhi iliendelea na siku alipoamua
kujiingiza kwenye uanamitindo kuna watu walimuuliza atamudu
kweli kufanya mitindo na hali aliyonayo?
"Nikiwa hapa nyumbani sikujua nasumbuliwa na nini. Siku moja
nikaamua kwenda kupima wakati huo nikiwa Afrika Kusini,
nikagundulika kuwa na ugonjwa wa Endometriosis na tiba pekee
ikawa kufanyiwa upasuaji," anasema Magese.
Anasema alifanyiwa upasuaji mara ya kwanza na kuonyesha yai
lake moja ni bovu hivyo kutakiwa litolewe ingawa alikuwa na
uwezo wa kubeba mimba.
"Nilifanyiwa upasuaji mara ya pili,kila siku nikalazimika kuwa
nafanyiwa uchunguzi ili kubaini maendeleo ya hali yangu, lakini
cha kushangaza hali ilizidi kuwa mbaya.Kuna wakati nilijiuliza
kwa nini mimi?" anasema Magese.
Anasema katika kipindi hicho alikuwa anachoma sindano kila
asubuhi kwa siku 63 ili kunusuru kizazi chake bila mafanikio,
aliendelea kufanyiwa upasuaji mara 12 zaidi.
Endometriosis ni nini? Dalili zake ni zipi?
Daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama na uzazi wa Hospitali
ya Taifa Muhimbili, Dr. Fadhlun Almy anasema bado hajapata jina
la Kiswahili la ugonjwa wa Endometriosis, lakini unasababishwa
na seli za tumbo la uzazi kuwa nje ya kizazi.
"Dalili za ugonjwa huu ni maumivu makali wakati wa hedhi na
maumivu hayo yanasababisha makovu ndani ya ukuta wa
tumbo.Makovu hayo yakizidi yanasababisha mirija ya uzazi
kuungana na Ovari," anasema
Tuko katika maboresho hivi karibuni blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma zetu za kutoa habari,tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi.
0 comments:
Post a Comment