Facebook

Thursday, 5 June 2014

Jamhuri ya kati yazuia huduma ya ujumbe mfupi (SMS) nchi nzima


Maafisa wanasema kuwa ujumbe mfupi ni tisho kwa usalama wa nchi
Maafisa wa utawala Katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, wamebana matumizi ya ujumbe mfupi wa simu za mkononi baada ya kusema kuwa ni tisho kwa usalama wa nchi.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa waziri wa mawasiliano serikali.
Watumiaji wa simu za mkononi ambao wamekuwa wakijaribu kutuma ujumbe mfupi wanapata jibu hili: ''Ujumbe wako hauwezi kutumwa.''
''Wenye simu za mkononi hawaruhusiwi kutuma ujumbe mfupi kuanzia Jumatatu 2 Juni hadi itakapotolewa taarifa zaidi kuhusu agizo hili,'' huu ndio ulikuwa ujumbe wa wizara ya mawasiliano kwa kampuni za kutoa huduma za simu.
Vurugu katika barabara za Bangui
Inaarifiwa kuwa uamuzi huo ulifikiwa na waziri mkuu Andre Nzapayeke.
Tangu wiki iliyopita, kumekuwa na ghasia zaidi mjini Bangui, pamoja na kutolewa wito wa maandamano uliotumwa kwa simu kama ujumbe mfupi siku chache zilizopita.
Duru zinasema kuwa hatua ya kubana ujumbe mfupi wa simu itadumu kwa siku kadhaa kabla ya agizo lengine kubatilisha amri hiyo.
Jamhuri ya Afrika ya Kati ambayo inakumbwa na vita kati ya jamii za wakristo na waisilamu imekuwa ikikumbwa na hali ngumu ya usalama pamoja na mashambulizi ya kulipiza kisasi kati ya jamii hizo.


Tuko katika maboresho hivi karibuni blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma zetu za kutoa habari,tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi.

0 comments:

Post a Comment