Mwanamuziki maarufu duniani
Justin Bieber, ameoamba radhi kwa kutumia neno la kibaguzi wakati
akiwakejeli wamarekani weusi kuhusu swala la ubaguzi wa rangi.
Bieber alitumia neno hilo "Nigger" katika kikao na marafiki zake alipokuwa anafanya vichekesho kuhusu swala la ubaguzi wa rangi.Jarida hilo linadai kuwa marafiki za Bieber wamekuwa na ufahamu kuhusu kanda hiyo na wamekuwa wakitumia pesa kujaribu kuificha.
Katika kanda hiyo Bieber anasikika akiuliza kwa nini wamarekani weusi wanaogopa misumeno inayotumia nishati.
Kanda hiyo inamalizika kwa Bieber kukejeli wamarekani wausi kwa kutoa sauti ya msumeno na kisha kurejelea kauli hiyo ya ''Kimbia Nigger'' mara tano.
Hata hivyo inasemekana kanda hiyo ilirekodiwa kama sehemu ya makala maalum kumhusu msanii huyo.
Justin Baieber na mwanamasumbwi Floyd Mayweather
Mapema jumatatu mwanamasumbwi, Floyd Mayweather, aliweka picha hii kwenye mtandao akiwa na Bierber kama ishara ya kumuunga mkono.
"Justin amekuwa mzuri sana kwangu na familia yangu. Sote ni binadamu na hufanya makosa , ni sehemu tu ya kuelekea katika utu uzima. Nina furaha kwa kile anachokifanya kama mwanamuziki na mfanyabiashara. ''
Tuko katika maboresho hivi karibuni blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma zetu za kutoa habari,tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi....stay tune....
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kupata taarifa mbalimbali zinazowahusu mastaa kwa muda na wakati muafaka.
0 comments:
Post a Comment