Kuna story zilisambaa baada ya ugomvi kati ya Solange na Jay Z ndani ya lift kuwa ndoa ya Jay Z na Beyonce imejaa vurugu kama uwanja wa vita na kwamba Jay Z anachepuka kivyake huku Beyonce nae akidaiwa kuchepuka na mlinzi wake.
Mchungaji Rudy Rasmus wa kanisa la St. John’s United Methodist ambalo alikuwa akisali Beyonce na familia yake pamoja na rafiki yake Kelly Rowland amefunguka kuhusu tuhuma hizo na anachokijua kuhusu uhusiano huo kwa sasa.
Akifanya interview na The Grio, mchungaji huyo ametofautiana kabisa na mawazo ya watu wengine na kueleza kuwa uhusiano kati ya wanandoa hao kwa sasa una nguvu kuliko kipindi chochote walichokuwa pamoja.
“Ni marafiki. Uhusiano wao una afya tele na maisha yao yameendelea kuwa mazuri.” Amekaririwa mchungaji Rudy ambaye pia ni mwanaharakati.
Amemtetea pia Beyonce kama muumini wa dini ya kikristo kwa kile ambacho amekuwa akikosolewa na waumini wa dini hiyo kuwa anaimba nyimbo za kidunia zilizo kinyume na matakwa ya Mungu.
Amesema Beyonce ni mburudishaji na kazi yake ni kuburudisha watu. Amewashangaa wanaomponda Beyonce kwa kuwa anachokifanya ni kuburudisha tu kama anavyofanya muigizaji kama Arnold Schwarzenegger.
Mhhh mchungaji anaacha maswali mengi kwani siku za hivi karibuni kuliibuka uvumi kuwa Beyonce ameanzisha dini yake na kuna watu wanamuabudu...
Tuko katika maboresho hivi karibuni
blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma zetu za
kutoa habari,tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi.
0 comments:
Post a Comment