Wasomi wanapokutana hasa katika zoezi la kutunukiwa cheti kama kielezo
cha uhitimu wa ngazi fulani kuna vitu huwezi kuvifikiria kama vitatokea
hata kidogo.
Katika Jack Britt High School, North Carolina, Marekani wanafunzi mmoja
amewaacha hoi mamia ya watu waliohudhuria sherehe ya kutunukiwa vyeti
(graduation) baada ya kupanda jukwaani kupokea cheti chake na ghafla
akavua johon lake na kubaki na boxer.
Baada ya kuvua joho alinyoosha mikono yote miwili juu kama mwanamieleka
anayetamba. Lakini haikuchukua round wanausalama wakamdhibiti na
kumuweka chini ya ulinzi.
Kwa mujibu wa The Huffington Post, kijana huyo alinyang’anywa diploma yake na hivyo hakukabithiwa cheti.
Hata hivyo bado anahesabiwa kama mtu aliye maliza masomo yake na kuhitimu licha ya kuwa hana kielelezo cha elimu yake.
“Shule yetu imefanya jitihada kubwa. Hapo zamani watu waliohudhuria
walikuwa wenye vurugu wakati wa graduation. Tumefanya jitihanda
kuwafanya watu waheshimu wanafunzi. Huyu kijana amechagua kutoonesha
heshima kwa wanafunzi wenzake.” Alisema Dr Frank Till, mwalimu wa chuo
hicho.
Tumehamia
katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali
kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi
vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com
0 comments:
Post a Comment