Muigizaji wa filamu nchini Yvonne Cherry maarufu kama Monalisa ambaye
pia aliwahi kuwa mke wa marehemu George Tyson aliyefariki dunia kwa
ajali ya gari wiki kadhaa zilizopita, amefunguka kupitia Instagram
kuelezea kusikitishwa kwake na ‘majungu’ ya watu kuwa hakustahili kupewa
pole kufuatia msiba huo.
Monalisa ameandika:
Let me clear the air.ni hivi,pamoja na ujinga tulioufanya mimi na
George ktk maisha yetu,kwa macho ya kibinadamu utasema alikuwa na mke
mwengine..bt kwa macho ya kiMungu mimi ni mke halali wa George Otieno
Okumu aliyelala.anayesema mke wa tyson alijifungia ndani mm nikawa
nachukua pole zisizo zangu,dah!kwanza wanawake walikuwa wawili ndani sio
mmoja.na wote walijifungia ndani,kwanini?ni wakristo na wanaijua
dini.waombolezaji waliokuwa wakinipa pole mimi,ni kwann?jiulize kabla ya
kuropoka halafu ww ni mwanamke kuna siku yatakukuta.nilienda kutimiza
wajibu wangu kama mke,ningelia peke yangu kwetu mngenisema sana,nimekaa
msibani naambiwa nachukuwa pole za bure.wacha nikukumbushe
maandiko…Alichokiunganisha Mungu?….;kilichofungwa
duniani?…..;nikupende,nikutunze hadi kifo?….. sasa kifo
kimetutenganisha.siku ya mwisho unadhani George ataitwa na nani?pamoja
na mambo yake yote wacheni nimlilie he was a good father kwa Sonia wangu
esp.miaka 5 ya mwisho wa uhai wake.acheni nimlilie he was my best
friend 1998-2014.nimeshare nae kitanda 2000-2006.nitakuwa mtu wa aina
gani nisiwe na uchungu?ukiona mwanamke mwenzio kaishindwa ndoa usimcheke
jua kuna sababu..na ni fundisho kwa wachukua waume za watu wote
mjini,mume akiumwa huwa anarudi kwa mkewe,na akifa?and for ur
info..msianze anajifanya mke ss hv ili apewe mali..Sonia ni mali kubwa
sana alioniachia am so happy.waaache wao wanaolilia kupewa pole
wapiganie.mwenyewe aliyetafuta kafa kaziacha sembuse tuliobaki?niacheni
nimlilie,waacheni fans wangu walie na mm.
George Tyson amezikwa jana Jumamosi ya June 15 kwao Kisumu Kenya.
Tumehamia
katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali
kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi
vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com
0 comments:
Post a Comment