Kocha
Jose Mourinho amekosoa nafasi aliyopangwa Wayne Rooney kwenye mechi ya
England na Italia huko Manaus, Brazil. Italia walishinda 2-1.
Rooney alitoa msaada mkubwa kwa Daniel Sturridge ambaye alifunga goli la kusawazisha huko Manaus ila uwezo wake wa pembeni ambao aliwekwa na kocha Roy Hodgson haukuweza kutoa msaada mkubwa kwa mshambuliaji pekee.
Na kocha wa Chelsea Mourinho, ambaye alijaribu kumsainisha Rooney msimu uliopita, alisema; “Sidhani kama ni nafasi nzuri kwa Rooney, ila mara nyingi wachezaji hawana budi kujitoa mhanga kwa ajili ya timu zao na nafikiri alifanya vizuri”.
Tumehamia
katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali
kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi
vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com
0 comments:
Post a Comment