Facebook

Sunday, 1 June 2014

Mwimbaji wa Marekani Ray J matatani....

Photo: RAY J MATATANI
Mwimbaji wa Marekani Ray J amekamatwa na polisi mjini Beverly Hills kwa tuhuma za kuzozana katika baa ya hoteli ya Beverly Wilshire.
Polisi wa Beverly Hills waliitwa baada ya kutokea malalamiko kuwa msanii huyo alimshika isivyo paswa mwanamke mmoja.
Wakati akitoka nje ya hoteli hiyo inadaiwa alipandwa na hasira na kugoma kuondoka.
Mtafaruku huo ulizidi kuwa mkubwa, na akalazimika kukamatwa. Inadaiwa Ray J alipiga teke kioo cha gari na kumtemea mate afisa wa polisi usoni.
Kwa mujibu wa tovuti ya TMZ, Ray J yuko nje kwa dhamana ya dola 20,000.
Ray J ni mdogo wake mwimbaji Brandy Norwood, na pia aliwahi kuwa mpenzi wake Kim Kardashian.

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kupata skendo mbalimbali za wasanii kwa wakati muafaka.

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment