Facebook

Saturday, 7 June 2014

Nyota wa Tennis mahakamani Afrika Kusini.

Madai dhidi ya Hewwit yanasemekana kutokea wakati alipokuwa kocha wa watoto
Mchezaji bingwa wa zamani wa Tennis duniani, Bob Hewitt amefikishwa mahakamani nchini Afrika Kusini kwa kosa la ubakaji na kuwanyanyasa watoto kijinsia.
Hii ni kwa mujibu wa mawakili wake.
Hewitt, ambaye kesi yake itaanza Februari mwaka 2015, amekanusha mashitaka matatu dhidi yake.
Mashitaka hayo yanahusiana na kipindi alichokuwa kocha wa watoto nchini Afrika Kusini mwaka 1980.
Bwana Hewitt, mwenye umri wa miaka 74, alishinda mataji tisa ya Grand Slam kwa wachezaji wawili kila upande katika miaka ya sitini na sabini.
Mzaliwa wa Australia , nyota huyo wa zamani wa Tennis alifikishwa katika mahakama ya Boksburg mjini Johannesburg, kwa mara ya kwanza Ijumaa.
Wakili wake aliambia mahakama kwamba mtuhumiwa alielewa fika madai yote dhidi yake na kusema anayakana yote matatu, mawili ya ubakaji na moja la unyanyasaji.
Vyombo vya habari nchini humo vimesema kuwa bwana Hewitt alionekana mnyonge na kwamba hata alisaidiwa kutembea wakati alipokwenda mahakamani.



Tuko katika maboresho hivi karibuni blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma zetu za kutoa habari na burudani.Tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi.Vitu vizuri vipya usivyotarajia utaviona na kufurahia kupitia www.bantutz.com....

Related Posts:

  • Mwimbaji wa Marekani Ray J matatani.... Mwimbaji wa Marekani Ray J amekamatwa na polisi mjini Beverly Hills kwa tuhuma za kuzozana katika baa ya hoteli ya Beverly Wilshire. Polisi wa Beverly Hills waliitwa baada ya kutokea malalamiko kuwa msanii huyo alimshi… Read More
  • Mtoto wa Pele jela miaka 33 Edinhio Pele alikuwa mlinda lango kabla ya kusataafu soka Mwanawe gwiji wa soka Brazil na duniani kote, Pele, Edinho Pele, amefungwa jela miaka 33 kwa kufanya biashara haramu ya pesa au kujipatia pesa chafu zilizoto… Read More
  • Unakijua alichokisema Nicki Minaj kuhusu kufunga ndoa na Drake  Nicki Minaj amejibu swali hili kwa uhakika kabisa bila wasiwasi wowote na kuwa gumzo tena.Minaj akiwa anafanya interview na magazine ya I-D moja ya majibu yake yana jadiliwa  hivi sasa kwenye internet. Jibu hil… Read More
  • Diamond aweka historia New Jersey  All Star Club Elizabeth New Jersey Diamond akikamua licha ya show kuchelewa kuanza na wapenzi wa Diamond kushikwa na jazba wakitaka aendelee lakini ikashindika kutokana na muda wa kufunga club kufika. &n… Read More
  • RAY C alitamani Penzi la kikongwe MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amesema kwa sasa hana mpango wa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu, na kama ikitokea basi atamtaka kuwa na miaka kuanzia 60. Akizungumza katika… Read More

0 comments:

Post a Comment