Picha zinazomwonyesha mh. Captain John Komba zenye mapozi tofauti na
mabinti tofauti zimeanza kusambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya
kijamii hapa Tanzania.
Kuna picha nyingine nyingi lakini kutokana na maadili hatuwezi kuziweka hadharani; hizi ni baadhi tu
UTETEZI WA KOMBA:
Kuhusiana na hizi picha 2 zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii kuznia
asubuhi ya leo, zikimuonyesha Mheshimiwa Mbunge huyo wa CCM Kapteni John
Komba akiwa kwenye mahaba na Mwanadada mmoja anayeishi Kinondoni.
Mbunge huyo amesema kwamba picha hizi zimetengenezwa na maadui wake wa
kisiasa na kwamba yeye sio Kiongozi wa hovyo hovyo namna hiyo.
Kapteni Komba amesema kwamba anawakaribisha wataalamu wa Picha na
Mitandao kutihibitisha ukweli wa picha hizo zinazoonyesha Mwana-Dada
akiwa na kipande cha khanga tu huku Mbunge huyo akiwa pembeni yake
akionyesha kutokuwepo kabisa kwenye Mahaba yanayotakiwa kuwa yanaendelea
baina yao.
Mbunge huyo ameuliza zaidi iweje awe kwenye mapenzi kama picha zinavyo
onyesha halafu awe na nguo zake zote huku msichana akiwa na khanga tu?
Kapteni Komba amesema kwamba kama kweli Taifa hili limefikia hapa pa
kuchafuana namna hii kisa mitizamo tofauti ya kisiasa ya namna ya
kuongoza Taifa letu basi kama Taifa tumefikia pabaya sana.
Mbunge huyo amemalizia kwa kusema kwamba wale wote wanaomuamini kama
Kiongozi shupavu wa Taifa, wasikatishwe tamaa na wajinga wachache wenye
mawazo ya kitumwa ambao wanadhani wanaweza kummaliza kisiasa kwa
kumtengenezea picha chafu kama hizi picha 2 za leo!
0 comments:
Post a Comment