Facebook

Wednesday, 4 June 2014

Umeisikia hii kuhusiana na Wanariadha wanaokunywa maziwa ya Matiti !!


Akina mama wakiwanyonyesha Matiti watoto wao
Wanariadha wanaume wamekiri kuanza kunywa maziwa ya Matiti kama njia ya kusisimua misuli yao badala ya kutumia madawa yaliyoharamishwa ambayo yanaongeza nguvu mwili.
Kwa mujibu wa jarida la Mail kwenye mtandao , wanyanyua uzani wengi wameanza kutumia maziwa ya matiti kama njia ya kujipatia nguvu.
Mwanariadha mmoja kutoka mjini New York kwa jina Antony, aliambia jarida la NYMag.com kwamba hukutana na wanariadha kadhaa ambao hunywa maziwa hayo ambayo wanasema ni mazuri na yanawapa nguvu.
Maziwa haya hununuliwa kwenye maduka ya mitandaoni ikiwemo mtandao ujulikanao kama 'Only the Breast and Human Milk 4 Human Babies' kwa dola mbini na nusu.
Baadhi ya wanaume wanasema maziwa ya Matiti inawapa nguvu za ajabu
Mwanariadha huyo anasema kuwa maziwa hayo humpa nguvu za ajabu.
Sababu ya wao kufanya hivyo , ni kujizuia kutumia madawa ambayo yamepigwa marufuku kwani wanaamini kuwa maziwa ya Matiti ni njia ya kiasili ya kuwapa nguvu.
Mwanariadha mmoja ambaye ni baba wa watoto wanne Jason Nash, anasema alianza kunywa maziwa ya mkewe baada ya mtoto wao wa kwanza kuzaliwa na akahisi kuwa ikiwa maziwa hayo ni mazuri kwa mtoto basi pia ni mazuri kwa watu wazima.
Ananukuliwa akisema kuwa maziwa hayo yamemlinda kutokana na magonjwa miaka hii yote.
Wanaume kadhaa wamezungumzia kunywa maziwa ya Matiti kama njia ya kuwapa nguvu badala ya kutumia madawa ya kusisimua misuli.
Wanaume ambao sio wanariadha wanasema maziwa ya Matiti yanawapa afya nzuri
Akijibu wakosoaji wake, wanaosema kuwa ni kitu cha ajabu na kushangaza, Antony alisema,'' mimi siamini madawa ya kusisimua misuli na ninataka vitu vya asili, ambavyo havina athari zozote mbaya kwa mwili.''
Wanaume wengine ambao sio wanaridaha ingawa wanakunywa maziwa ya Matit, wanasema kuwa maziwa hayo huwafanya kujisikia kama walio na nguvu mno na wenye afya tele.
David,mwenye umri wa miaka 42, kutoka Brooklyn, aliambia jarida hilo kuwa alianza kunywa maziwa ya matiti miaka mitatu iliyopita. Alisema ilisabidia sana wakati alipokuwa anapokea matibabu ya Saratani kwa kuwa alikuwa anahisi kutapika wakati wote alipokuwa anapokea matibabu.
Pindi alipokunywa maziwa hayo hisia za kutapika wakati wote zilimtoka
Alisema maziwa hayo ambayo ni matamu , yalimsaidia sana.

 Tuko katika maboresho hivi karibuni blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma zetu za kutoa habari,tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi.

Related Posts:

  • Congo watangaza hatua mpya za kupambana na Ebola.Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetangaza hatua mpya za kupambana na ugonjwa wa Ebola wiki 3 baada ya ugonjwa huo kuwauwa watu 32 miongoni mwa 59 waliombukizwa na virusi hivyo.Waziri wa Afya nchini humo amesema … Read More
  • Wafungwa wapigwa risasi mahakamani Afrika Kusini.Wafungwa wawili wamepigwa risasi walipokuwa wakijaribu kutoroka kutoka katika mahakama moja nchini Afrika Kusini. Afisa mmoja kutoka wizara ya sheria aliambia chama cha wanahabari nchini humo kwamba wafungwa waliokuwa wanasub… Read More
  • Tahadhari kuhusu gesi za sumuMkuu wa shirika la utabiri wa hali ya anga la Umoja wa Mataifa Michel Jarraud, ametoa tahadharti kuwa dunia nzima inapaswa kushughulikia mabadiliko ya hali ya anga haraka iwezekanavyo la sivyo muda unakwisha. Takwimu mpya kut… Read More
  • WAPENZI WA JINSIA MOJA WAFUNGA NDOA BAADA YA KUISHI PAMOJA MIAKA 72Zaidi ya miongo sabini baada ya kuanza uhusiano wa kimapenzi, Vivian Boyack na Alice "Nonie" Dubes wamefunga ndoa. Boyack, 91, na Dubes, 90, walifunga ndoa rasmi Jumamosi iliyopita, limeripoti gazeti la Quad City Times. "Sher… Read More
  • Nyama ya Kiboko yawaletea maafa Afrika KusiniWatu kumi walikanyagwa na gari lililokuwa linakwenda kwa mwendo wa kasi walipokuwa wanajaribu kujipatia angalau kipande cha nyama ya Kiboko mwishoni mwa wiki. Taarifa hii ni kwa mujibu wa mtandao wa Daily Nation. Kiboko huyo … Read More

0 comments:

Post a Comment