Wanasayansi nchini Uingereza
wanasema kuwa inawezekana kwa wao kuwazalisha watoto kutoka kwa wazazi
watatu katika kipindi cha miaka miwili ijayo.
Wanasayansi hao wanasema kuwa wanasubiri
mabadiliko katika sheria na badiliko katika mtazamo ya watu kabla
hawajapandikiza manii kwa mayai kutoka kwa wanawake wawili .Hata hivyo mipango hiyo tayari imevutia tahadhari kutoka kwa halmashauri inayosimamia utabibu wa uzazi nchini Uingereza.
Takwimu nchini Uingereza zinaonesha kati ya watoto 6500 wanaozaliwa kuna mmoja aliyeambukizwa maradhi kutoka kwa wazazi wake kupitia celi zijulikanazo kama (mitochondria.) ambazo zinasababisha maradhi kama kukosa nguvu mwilini kupofuka maradhi ya moyo na hata wengine hufa.
Watafiti na madaktari wa maswala ya uzazi chini ya nembo ya Human Fertilisation and Embryology Authority (HFEA)waliohudhuria kongamano hilo walishuhudia hatua kwa hatua jinsi utaalamu huu unaweza kumsaidia mama ambaye anaseli za mwili zilizoambukizwa akisaidiwa kumzaa mtoto bila ya maradhi hayo kwa usaidizi wa mwanamke mwenye seli nadhifu na yenye afya.
Serikali kwa upande wake imeipungia teknolojia hii kwani itaisaidia jamii kutoathirika na magonjwa ambayo hurithishwa kutoka kwa mama hadi kwa mtoto.
Daktari mkuu , Prof Dame Sally Davies, akisema ni jambo la dharura ambalo serikali inasubiri tu kuafiki utafiti huo na kisha kupitisha sheria zitakazoruhusu watoto wenye wazazi watatu.
Tuko katika maboresho hivi karibuni blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma zetu za kutoa habari,tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi.
0 comments:
Post a Comment