Facebook

Thursday, 5 June 2014

Baada ya Nick wa Pili Kusifiwa bungeni,Ney wa Mitego, Shilole, Wema na Aunt Ezekiel wapondwa.


Bungeni: Baada ya Nick wa Pili Kusifiwa, Nay wa Mitego, Shilole, Wema na Aunt Ezekiel Watajwa Kivingine

Baada ya kuonekana kuwa ukiukwaji wa maadili Tanzania ni miongoni mwa majanga ya kitaifa yanayotakiwa kupigiwa filimbi ya hatari mapema kuokoa kizazi hiki, serikali imenyoosha mkono wake kwa baadhi ya wasanii na waburudishaji walioonekana kuwa sehemu ya tatizo hili.
Wema Sepetu nzuri
Akijibu swali lilioulizwa jana bungeni na mbunge Catheline Magige, Naibu Waziri wa habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Juma Nkamia alifafanua hatua zilizochukuliwa na serikali kupitia wizara yake kuhakikisha wanakomesha mapema vitendo hivyo.
Nkamia alieleza kuwa serikali ilishafanya vikao na wamiliki wa kumbi mbalimbali za starehe, wamiliki wa bendi, maafisa utamaduni na wakuu wa jeshi la polisi.
Baada ya vikao hivyo, serikali ilizuia kutoa kibali kwa vikundi vya Kangamoko kutokana na jinsi vikundi hivyo vinavyotumbuiza kwa mitindo inayokiuka maadili ya Tannzania na pia wametoa onyo kwa wasanii wa filamu na muziki wa kizazi kipya.
“Mfano wasanii waliopewa onyo ni Nay wa Mitego, Shilole na Anti Ezekiel. Na kwa upande wa kumbi ni Mamas &Papas.” Nkamia ameeleza.
aunt ezekiel onyoshilole kiunoNAY WA MITEGOO TIMES FM
Ameongeza kuwa serikali imeunda kamati ya kitaifa ya kuzuia vitendo vya ukatili, unyanyasaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi na watoto, na vitendo vyote vya udhalilishaji wa wanawake.
Wiki kadhaa zilizopita, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka alimsifia Nikki wa Pili kupitia wimbo wake wa Staki Kazi kama mfano wa kuigwa kwa vijana wanaotegemea kuajiriwa.



Tuko katika maboresho hivi karibuni blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma zetu za kutoa habari,tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi.

0 comments:

Post a Comment