Katika hali isiyo ya kawaida Diamond Platnumz azidi kutokewa na
bahati kila siku, ila kwa hili si bahati tu,ila ni zaidi ya bahati kwa sababu
haijawahi kutoke kwa mwanamuziki yeyote mwingine hapa east africa.
Story nzim ilikuwa hivi;Mapema alhamisi ya wiki hii Diamond platnumz
alikutana na manager wa televisheni ya kimataifa ya Channel O, Diamond
akiwa anahojiwa na kipindi kimoja cha redio alizidi kufunguka zaidi na
kusema , alipokutana na manager huyo, alipata nafasi ya kumuonyesha
video yake mpya aliyoifanya huko uingereza, ile kuiona tu hakuamini kuwa
kuna vitu adimu kama hivi huku east africa, na kumuomba Diamond hapo
hapo aweze kumpa uwezo wa kuicheza exclusive (kwa mara ya kwanza) video
hiyo Channel O, Diamond aliona kama utani hivi ila bada ya kuongea na
producer wa video hiyo, ambaye ndiye aliyeitengeneza video yake ya my
number one remix aitwaye Clarence, alimpa meneja huyo wa Channel O na
baada ya muda, alishtuka kuona watu wakimtumia ujumbe kumpa hongera
kutokana na video hiyo jinsi ilivyo kali baada ya kupigwa Channel O.
“Ilikuwa tuitoe officialy kwenye media baada ya tuzo hizi kuisha na
tulisubiri muda mzuri wa kuachia video hiyo, ila imetokea kama bahati ya
kuombwa video hiyo kupigwa exclusive katika channel O, cause walisema
lete tuipige kipindi hiki, tuonyeshe vipaji vilivyotoka east africa, na
nashukuru kwa hilo, ila naona officialy hivi karibuni itabidi niitoe
pamoja na nyimbo yake”- alimalizia Diamond Platnumz
Tuko katika maboresho hivi karibuni
blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za
kuboresha huduma zetu za kutoa habari na burudani.Tutakuja katika muonekano
mpya na bora zaidi.Vitu vizuri vipya usivyotarajia utaviona na kufurahia
kupitia www.bantutz.com....
0 comments:
Post a Comment