Msanii anaeunda kundi la Wagosi wa Kaya kutoka Tanga, Dkt John amenusurika kifo katika ajali mbaya iliyohusisha pikipiki na gari dogo eneo la Barabara ya Nane, Tanga.
Dkt John ameeleza kuwa alikuwa anaendesha pikipiki katika mitaa ya Tanga jana majira ya mchana kwa kuwa gari lake likuwa kwa fundi likibadilishwa bodi, lakini alikutana na gari dogo ambalo dereva wake alichelea kuzifuata sheria za barabarani na kusababisha ajali.
“Jamaa alikuwepo mbele yangu yeye hakuwasha endicator kama anakata kulia kuelekea kwenye ofisi ya Raha Leo, matokeo yake mimi nikajua ananyoosha atapita kwenye soko la Ngamiani. Mimi nikajichanganya kwenye 18, kumbe jamaa wala hanyooshi wala nini anakata bwana. Kwa hiyo akawa anakata halafu ndio anawasha indicator. Kwa hiyo akanipush…nikamvaa akanipush.”
Ameeleza kuwa alipata jeraha kubwa katika mguu wake wa kushoto bada ya kidonda kuchimbika nusra aguswe katika mfupa na ameshonwa nyuzi nane.
“Goti limevunjika kidogo, kwa hiyo kesho nategemea kupata transfer kwa ajili ya kuelekea Muhimbili ili nikatibiwe, kama itakuwa hivyo kwa sababu kuna daktari mmoja ndio tunaemsubiria, kama atakuwa hajarudi itabidi nikatibiwe Muhimbili kama wiki sita hivi.”
Tuko katika maboresho hivi karibuni
blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma zetu za
kutoa habari,tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi.
0 comments:
Post a Comment