Facebook

Tuesday, 3 June 2014

Hatimaye familia ya mwanafunzi aliyefariki Chuo Kikuu cha DSM yaeleza ukweli kuhusu kifo chake !

 

Hatimaye familia ya mwanafunzi  wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, marehemu Happy Sekabenga Pius Mwakimenya (21) kilichotokea hivi karibuni na kugubikwa na utata, imeanika ukweli kuhusiana na tukio hilo.

Akizungumza na mtandao huu
, mwishoni mwa wiki iliyopita katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, baba mdogo wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Joseph Mwigune alisema, taarifa waliyopewa na daktari aliyemfanyia uchunguzi inamaliza utata na minong’ono yote inayoendelea chuoni.
Mwili wa marehemu Sekabenga Pius Mwakimenya ukiwa kwenye jeneza.
Alisema, kwa mujibu wa ripoti hiyo, kifo cha Sekabenga kimetokana na mzunguko wa damu katika mishipa kutokuwa sawa, jambo lililosababisha ajisikie vibaya na hatimaye kufariki dunia.

Daktari amesema kwamba mishipa ya damu haikuwa ikifanya kazi vizuri hali iliyomsababishia ajisikie kuchoka kwa sababu damu haikuwa ikifika sehemu zote za mwili wa marehemu,” alisema Mwigune.
Sekabenga akiagwa.
  www.bantutz.com lilifunga safari hadi chuoni na kuzungumza na baadhi ya wanafunzi ambao walionyesha wasiwasi kuwa huenda marehemu aliamua kujiua kwa sumu kwa maelezo kuwa, siku chache kabla ya kifo chake alionekana mwenye mawazo mengi.

Hakuwa mwenye furaha, ni kama alikuwa na jambo zito linalomsumbua ndiyo maana unasikia wanafunzi wengi hapa chuoni wanahusisha kifo chake na sumu,” alisema mwanafunzi  mmoja kwa sharti la kutotajwa jina lake.
Mwili wa Sekabenga ukiingizwa kwenye gari.
Hata hivyo, taarifa kutoka kwa familia inayonukuu ripoti ya daktari inaziba minong’ono yote kwa kuwa haionyeshi mahali popote kuwa marehemu alijiua kwa sumu.

Marehemu Sekabenga alikuwa mwaka wa pili chuoni hapo  akichukua Shahada ya Kwanza ya Biashara na Uhasibu, mwili wake  umesafirishwa Jumamosi Mei 31, mwaka huu kwenda mkoani Mbeya kwa maziko yaliyotarajiwa kufanyika jana Jumatatu.


kama haukusoma habari ya mwanzo iliyokuwa inaelezea tukio jinsi lilivyokuwa,kwa kuangalia video na picha mbalimbali kipindi mwili wa marehemu unatolewa katika chumba cha kulala wanafunzi (hostel) unaweza kufuatilia hapa chini.

Bofya hapa
< <Habari kuhusiana na Kifo Cha Happy Sekabenga>>


Tuko katika maboresho hivi karibuni blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma zetu za kutoa habari na burudani,tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi hivi karibuni.Utaweza kufuatilia mechi zote live hususan za kombe la dunia kupitia site yetu mpya,Utapa notifications ya habari mpya kupitia simu yako ya mkononi bila makato yoyote, utaweza kudownload na kusikiliza nyimbo mpya katika blog yetu na Utaweza kudownload application ya blog yetu iwe katika simu yako na siku za karibuni itakuwa  PLAYSTORE.
Kuwa wa kwanza ku-like page ya site yetu mpya hapa <<bantutz.com/facebookpage>>
          www.bantutz.com-Instant Updates and Entertainment

0 comments:

Post a Comment