Wapenzi wangu najua kila kitu kilianzia kwenye leo tena hadi wewe kuamua
kufatilia kazi zangu na kila kitu ninachofanya.Ila wanasema safari moja
huanzisha nyingine ndivyo ilivyo kwangu.
Baada ya muda wa miaka nane kuongoza leo tena na mie kuilea kwa kila
hali kuhakikisha inakuwepo.Leo tena ilikuwa maisha yangu
nikilala,nikiamka,nikiwa barabarani ili mradi niwe na jambo kwa
msikilizaji wangu kila siku.Iwe ni segment mpya,topic,wimbo,jingle,yaani
chochote ambacho naona kitanogesha kipindi.
Nilichukua likizo ya martenity na niliporejea nikaambiwa dada
tunakuhamishia sehemu nyingine,TV.Daah haikuwa kazi rahisi kukubali na
kuipokea niliona daah itakuwaje jamani mbona leo tena ndio kila kitu
kwangu.
Nikaelezwa vile ofisi ina malengo makubwa na kipindi kipya
nitakachoanzisha ambayo siwezi kuyaanika hapa lol basi kidogo kidogo
nikaanza kuelewa somo na sasa nipo tayari.Kuna wale ambao bado
mnaendelea kuulizia kwa nini hamnisikii ukweli ndio huo kwa sasa sipo
tena kwenye leo tena najiandaa na kipindi changu kipya cha tv
kitakachoruka clouds tv hapo baadae.
Japo nina changamoto ya mwili mmenenepa mie ila kila kitu kitajiset
mbele ya safati.Nikiwa najiandaa na kipindi kipya pia najiaandaa na ule
utaratibu wangu wa kusaidia watoto yatima kupitia dada dina cares ambayo
itakuwa ni mwezi ujao.
Najua tayari nina mawazo yangu ya nini nitafanya kwenye hicho kipindi
lakini pia naomba nikuulize.Ungependa kuona nini kwenye kipindi changu
cha tv?
Tuko katika maboresho hivi karibuni
blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za
kuboresha huduma zetu za kutoa habari,tutakuja katika muonekano mpya na bora
zaidi.
0 comments:
Post a Comment