BAADA
ya kumnyaka Straika hatari wa Atletico Madrid, Diego Costa, sasa
Chelsea wanaimarika zaidi kwa kumnasa Kiungo wa Barcelona Cesc Fabregas
ambae Watu wa karibu yake wamethibitisha kuwa anarudi Ligi Kuu England
akiwa Stamford Bridge.
Kuondoka kwa Fabregas huko Nou Camp
kumethibitika hasa baada ya Beki wa Barca, Gerard Pique, kuropoka mbele
ya Kipaza Sauti bila kujijua wakati akiongea na Kocha wa Spain, Vicente
Del Bosque, huko Washington DC, Marekani alipomwambia Kocha wake:
“Ameniambia anaondoka. Anakwenda. Ameniambia Milioni 33.”
Del Bosque akajibu kwamba hizo ni habari mbaya kwa Rais wa Barca, Josep Maria Bartomeu.
Hata hivyo, Pique hakutoboa wapi Fabregas anakwenda lakini huko London Vyombo vya Habari vimedodosa na kubaini ni Chelsea.
Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho,
anasaka Kiungo wa kumbadili Mkongwe Frank Lampard ambae ameshatangaza
kuondoka Stamford Bridge na inaelekea atajiunga na MLS kwenye Klabu ya
New York City.
Fabregas alianza Soka lake huko Barca na
kuhamia Arsenal Mwaka 2003 akiwa na Miaka 15 na alichezea Klabu hiyo
Mechi 305 na kufunga Bao 59.
Mwaka 2011, Fabregas alirudi Barca na kuweza kutwaa La Liga na Copa Del Rey mara moja kila moja.
Tuko katika maboresho hivi karibuni
blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za
kuboresha huduma zetu za kutoa habari,tutakuja katika muonekano mpya na bora
zaidi.
0 comments:
Post a Comment