MKONGWE kwenye sanaa za Kibongo, Blandina Chegula ‘Johari’ amesema
kufuatia vifo vya mfululizo vya wasanii, kwa kiasi kikubwa wasanii
wamebadilika kitabia
Akipiga stori na paparazi wetu alisema, wasanii hao wamejitambua kuwa
duniani watu wanapita, jambo ambalo kwa muda mrefu walikuwa wamelisahau
na kuponda raha mfululizo.
“Tangu wenzetu wafariki mfululizo, wasanii wengi tumepata mshtuko na
kujitambua, naona wengi wamebadilika, wamenyooka na kuanza kumrudia
Mungu,” alisema Johari.
Vifo vya wasanii vilivyotokea hivi karibuni ni pamoja na cha Adam Kuambina, Sheila Haule ‘Recho’ na George Tyson.
Tuko katika maboresho hivi karibuni
blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za
kuboresha huduma zetu za kutoa habari na burudani.Tutakuja katika muonekano
mpya na bora zaidi.Vitu vizuri vipya usivyotarajia utaviona na kufurahia
kupitia www.bantutz.com....
0 comments:
Post a Comment