Facebook

Monday, 9 June 2014

Rais Jacob Zuma alazwa hospitalini

Rais Zuma anatarajiwa kupumzika kwa muda kabla ya kurejea kazini
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amelazwa hospitalini kwa uchunguzi wa kiafya .
Taarifa hii ni kwa mujibu wa maafisa kutoka kwa ofisi yake. Taarifa hiyo ilisema kuwa Zuma atalazimika kumpumzika kwa muda ingawa ataendelea na majukumu yake ya kitaifa akiwa nyumbani.
“Hapo jana Ijumaa Rais Zuma alishauriwa kupumzika hasa baada ya msimu wa uchaguzi kukamilika wiki chache zilizopita.Madaktari hawajaeleza wasiwasi wowote kuhusu afya yake.’’
Bwana Zuma ambaye alihusika na harakati dhidi ya utawala wa kibaguzi, ana umri wa miaka 72 na aliapishwa kwa muhula wa pili baada ya uchaguzi mkuu tarehe 24 mwezi Mei, ambapo chama chake ANC kilishinda uchaguzi huo.
Baraza lake la mawaziri, lina kibarua kigumu kukabiliana na uchumi wa nchi hiyo unaoendelea kudorora kila kukicha pamoja na ukosefu wa ajira.
Wadadisi wanasema asilimia 25 ya wananchi hawana ajira.



Tuko katika maboresho hivi karibuni blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma zetu za kutoa habari na burudani.Tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi.Vitu vizuri vipya usivyotarajia utaviona na kufurahia kupitia www.bantutz.com....


Related Posts:

0 comments:

Post a Comment