Kamanda wa Polisi Kanda ya Temeke Engelbath Kiondo leo amezungumza na
vyombo mbalimbali vya habari ofisini kwake kuelezea kilichotokea jana
kwenye uzinduzi wa radio hiyo mpya ya 93.7 E-FM.
Kamanda huyo alisema Jeshi la Polisi na waandaji wa tamasha hilo
walipoona umati wa watu kuwa mwingi na ili kuepusha madhara ambayo
yangeweza kujitokeza kwa rai basi walizima mzuki mapema nusu saa kabla
ya kumalizika kwa shughuri hiyo.
Hata kitendo cha kuzima muziki kabla ya muda kumalizika kiliwauzi vijana
ambao walionekana ni wahuni ambao walianza kurusha mawe kwenye jukwaa
pamoja na kuwashambulia Polisi kwa mawe ndipo polisi walitumia nguvu za
ziada za kuwatawanya vijana hao wa kihuni kwa kuwarushia mabomu ya
machozi.
Aidha katika taarifa yake Kamanda huyo alisema kuwa katika purukushani
hizo polisi watatu wameumia lakini wanaendelea vizuri hadi sasa.
Tuko katika
maboresho hivi karibuni blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma
zetu za kutoa habari,tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi.
0 comments:
Post a Comment