Mitandao mingi ya udaku wamekuwa wakiripoti mapenzi mapya kati ya rapper wa Bad Boys record “French Montana” na “Khloe Kardashian” ambaye ni mdogo wake Kim Kardashian.
Khloe alikuwa ni mke wa mcheza kikapu Lamar Odom lakini wamepitia mambo mengi na jinsi ilivyo hivi sasa mahusiano yao hayapo vizuri kabisa.
Sasa kilichotokea hivi sasa ni kwamba Khloe Kardashian amesafiri hadi South Africa kuungana na French Montana ambaye anatarajiwa kufanya show kwenye tukio hilo.
Sifa moja wapo ya mtu yoyote anayekuwa na mahusiano na Kardashian sisters lazima ataandamwa na vyombo vya habari sana haswa mapaparazi. Kanye West alikuwa anasumbuliwa na mapaparazi lakini hali ilizidi baada ya kuanzisha mahusiano na Kim K.
Sasa French Montana na yeye ameshaanza kuandikwa na kupigwa picha na mitandao mingi sana.
Tuko katika maboresho hivi karibuni
blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za
kuboresha huduma zetu za kutoa habari na burudani.Tutakuja katika muonekano
mpya na bora zaidi.Vitu vizuri vipya usivyotarajia utaviona na kufurahia
kupitia www.bantutz.com....
0 comments:
Post a Comment