Mwanamuziki wa zamani na mbunge Vicky Kamata baada ya ndoa yake kudaiwa
kuzuiliwa kufungwa kutokana na kudaiwa mwanaume aliyetaka kufunga naye
ndoa ana ndoa nyingine, amefunguka kwa kudai kuwa hizo zilikuwa ni
habari za kutungwa na hazikuwa na ukweli wowote.
Vicky alikuwa anahojiwa na kituo cha redio nchini jana alisema kuwa maneno mengi ambayo
yalikuwa yanazungumzwa kuhusu ndoa yake kutofungwa yalikuwa
yametengenezwa na watu.
“Kweli ni maradhi kama ambavyo ilitangazwa wakati huo, lakini pamoja
na hayo mimi bado nasema Mungu alikuwa hajapanga ,alikuwa hajaruhusu
kuwa tarehe 24 mwezi wa tano iwe siku wa kufunga ndoa.
“Mimi kama binadamu na mwenzangu tulipanga lakini mungu alipanga
vinginevyo , kwaiyo siku zote mapenzi ya mungu huwaga yanatimia siyo
mapenzi ya binadamu.
“Ni kweli alishawai kufunga ndoa lakini ninachofahamu mimi ni kwamba
waliachana kihalali kabisa kwa divorce ya mahakama ya Kinondoni mwaka
2012 na mimi siyo mtoto mdogo kwamba ninaweza mpaka nikafikia hatua hiyo
bila kuwa nimemchunguza huyo mtu.
“Kuhusu swala la kwamba alikuwa na mke wake , mke wake alikwenda
kuzuia Kanisani sijui alikuja Bungeni, yale yalikuwa tu ni maneno ambayo
yalitengenezwa na baadhi ya watu kwa interest zao ,lakini siyo kwamba
nilikuwa nimeingilia ndoa ya mtu hata kidogo, kwa sababu ata huyo mke wa
kwanza wa huyo aliyekuwa mchumba wangu aliongea na vyombo vya habari
akasema mimi sijaenda Dodoma wala sijaenda kuzuia harusi.
“Kwaiyo maneno yaliyokuwa yamezagaa ,sijui mke wake amezuia yalikuwa
ni maneno ya kutengenezwa na watu tu kwa nia zao wenyewe lakini siyo
kweli.
“Kuhusu kwamba hajulikani alipo mimi hilo siwezi kumjibia, mimi
nafahamu kwamba yupo na anaendelea na shughuli zake kama kawaida, kama
ambavyo mimi naendelea na shughuli zangu kama kawaida, tunawasiliana,
yani cha kufahamu tu kwamba ndoa haikufungwa basi.
“Hata kama kuna mkono wa binadamu katika jambo hilo mimi naamini
mungu ndo mwenye mamlaka na Mungu ndiyo mwenye kupanga mambo, kwaiyo
kama Mungu alikuwa anataka hiyo harusi ifugwe ata kama kungekuwa na
binadamu mwingine hataki bado ingefungwa…
“Kwaiyo mimi sitaki kuamini sana kwamba kuna waheshimiwa wabunge
wenzangu wamechangia kwa kiasi kikubwa kwamba ndoa ile isifungwe, mimi
ninaamini ni mapenzi ya Mungu tu yametimizwa kwa staili hiyo” Alisema Vicky.
Tuko katika maboresho hivi karibuni
blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za
kuboresha huduma zetu za kutoa habari,tutakuja katika muonekano mpya na bora
zaidi.
0 comments:
Post a Comment