Facebook

Saturday, 7 June 2014

Kilichomuua ‘Mtoto wa Boksi’ Chabainika; wahusika kunyongwa!

Kufuatia kifo cha mtoto Nasra, almaarufu kama ‘mtoto wa boksi’, kuna kila dalili kwamba kifo chake kimetokana na maradhi aliyoyapata wakati akiwa anaishi kwenye boksi. Kwa kuwa imethibitika kwamba mtoto alifariki kutokana na ugonjwa wa pumu—kufuatia kufungiwa kwenye mazingira machafu, kutoogeshwa na kupigwa na baridi masaa 24, na kwa kuwa wahusika waliokuwa wakimfanyia ukatili huo tayari walishakamatwa na kufunguliwa mashitaka ya kula njama za kumtesa mtoto huyo mdogo asiyekuwa na hatia na asiyeweza kujitetea, mawakili wanaosimamia kesi hii watabadilisha masitaka ya kesi na kuwa KESI YA MAUAJI YA KUKUSUDIA.

Adhabu kwa mtu anayeua kwa kukusudia ni KUNYONGWA MPAKA KUFA. Kwa hiyo, wahusika wanasubiri kunyongwa hadi kufa pindi hukumu ya kesi hii itakapotoka. Na kwa kuwa kuna ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani hawa wanadamu wasokuwa na haya, wajiandae kupokea kitanzi ili liwe fundisho kwa washenzy wengine wenye tabia za kinyama kawa hawa wendawazimu.

Tuko katika maboresho hivi karibuni blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma zetu za kutoa habari na burudani.Tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi.Vitu vizuri vipya usivyotarajia utaviona na kufurahia kupitia www.bantutz.com....

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment