Facebook

Friday, 6 June 2014

Kiongozi wa waisilamu afariki dunia Nigeria


Marehemu Emir Al-Haji Ado Bayero
Kiongozi wa waisilamu katika jimbo la Kano nchini Ngeria,Al-Haji Ado Bayero, amefariki.
Kiongozi huyo mwenye kuheshimiwa sana miongoni mwa viongozi wengine wote nchini humo , amethibitishwa kufariki nchini humo.
Al-Haji Ado Bayero, alikuwa mtawala wa Kano tangu mwaka 1963 na alifariki baada ya kuugua kwa mda mrefu.
Tangu wakati huo Nigeria imekabiliana na misukosuko ya mapinduzi ya kijeshi na ghasia zingine.
Alikuwa na umri wa miaka 84 na kutambuliwa kama kiongozi wa muda mrefu sana na mkongwe zaidi wa waisilamu katika jimbo hilo na pia alitambulika kama kiongozi wa pili mwenye ushaiwishi zaidi kwa waisilamu Nigeria
Marehemu Emir pia alitambuliwa kama kiongozi aliyependa amani.
Miaka miwili iliyopita alinusurika kwa tundu la sindano baada ya msafara wake kushambuliwa ambapo dereva wake na walinzi wake wawili walifariki.
Ilishukiwa kuwa kundi la wapiganaji wa kiisilamu wenye itikadi kali, Boko Haram, ndio waliomshambulia.
Boko Haram wamewashutumu viongozi wa kijadi nchini Nigeria kwa kuwa vibaraka wa wanasiasa. Juma lililopita Emir wa Gwoza aliuliwa na kundi hilo ambalo limetekeleza mashambulizi mengi Kaskazini Mashariki mwa nnchi hiyo.
Mwandishi mmoja mjini Abuja anasema kuwa emiralikuwa amerejea tu kutoka mjini London ambako alikuwa anapokea matibabu.
Maishani mwake alikuwa mfanyakazi wa banki, polisi, mbunge , balozi na mfanyabiashara maarufu.



Tuko katika maboresho hivi karibuni blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma zetu za kutoa habari,tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi.


0 comments:

Post a Comment