Kwa ushindi wa Profesa Mutharika katika kiti cha urais wa Malawi,
anaongeza idadi ya jamii ya wasomi waliopitia Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM), ama wakiwa wahadhiri au wanafunzi, kwani alifundisha
chuoni hapo mwishoni mwa miaka ya 1960 na mwanzoni mwa miaka ya 1970.
Nje ya kazi za uhadhiri, Profesa Mutharika aliyebobea katika masuala ya
sheria ambaye pia ni mwanasiasa mzoefu na mashuhuri, ameshika nyadhifa
za uwaziri katika wizara mbalimbali zikiwamo Wizara ya Sheria, Wizara ya
Mambo ya Nje na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, nafasi
aliyoishika hadi anaingia katika uchaguzi mkuu hivi karibuni.
Mbali ya Profesa Mutharika, wasomi wengine waliopitia UDSM na kufanikiwa
katika ulingo wa kisiasa na hata kuwa marais au viongozi waandamizi
katika nchi zao ni Rais Jakaya Kikwete, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni,
Rais wa zamani wa Zaire (sasa DRC) Laurent Desire-Kabila.
Aidha, Makamu wa Rais wa zamani wa Uganda, Eriya Kategaya alisoma Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam, kama ilivyo kwa aliyekuwa Makamu wa Rais wa
Sudan, John Garang.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro ambaye kwa
sasa ni Waziri wa Sheria na Katiba, naye alisoma Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam kama ilivyo kwa Mawaziri wakuu watatu wa Tanzania, Jaji Joseph
Sinde Warioba, Edward Lowassa na Mizengo Pinda.
Getrude Mongella, Rais wa zamani wa Bunge la Afrika ambaye pia alishika
wadhifa wa Katibu Mkuu wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya
Wanawake Duniani uliofanyika Beijing, China mwaka 1995.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa sasa wa Tanzania,naye amesoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Watu wengine mashuhuri waliosoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni pamoja
na mwanasheria Mkuu wa Kenya, Dk Willy Mutunga na Donald Kaberuka, Rais
wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) ambaye ni raia wa Rwanda.
0 comments:
Post a Comment