Facebook

Monday, 16 June 2014

kundi la Taleban lawakata vidole waliopiga kura.



Raia waliopiga kura nchini Afghanistan wakatwa vidole
Maafisa nchini Afghanistan wanasema kuwa watu 11 wamefariki akiwemo mwangalizi mmoja wa uchaguzi baada ya gari lao kazkazini mwa taifa hilo kukanyaga bomu lililotegwa barabarani siku moja tu baada ya kuanza kwa uchaguzi wa urais wa raundi ya pili.
 
Katika tukio jengine kundi la Taleban liliwakata vidole baadhi ya raia kama adhabu ya kushiriki katika uchaguzi nchini humo.
Zaidi ya watu 60 wameuawa na wanamgambo hao katika misururu ya mashambulizi wakati wa raundi ya pili ya uchaguzi wa urais.
Raia wa taifa hilo wanachagua kati ya aliyekuwa waziri wa maswala ya kigeni Abdulla Abdulla na Ashraf Ghani ambaye aliwahi kuhudumu kama waziri wa fedha.
Wagombea wote wameahidi kuimarisha uhusiano na mataifa ya magharibi mbali na kukabiliana na ufisadi.


Tumehamia katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com

Related Posts:

  • Boko Haram wauteka mji mkubwa wenye,watu wengi Nigeria.Wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram wameuzingira mji wa Maiduguri , mji rasmi wa jimbo la Borno Kaskazini Mashariki ya Nigeria. Wazee wa vijiji wametahadharisha kuwa jeshi linahitaji kuweka ulinzi thabiditi katika mji huo a… Read More
  • Mwanaume apata dalili za ujauzito Uingereza.Harry Ashby ni mwanaume wa kwanza nchini Birmingham kupata ruhusa ya kupumzika nyumbani baada ya kusumbuliwa na homa mithili ya mwanamke mja mzito. Amekuwa akipatwa na homa za vipindi hasa nyakati za asubuhi baada ya mchumba … Read More
  • Mahakama yazuia unywaji Pombe India. Mahakama ya rufaa nchini India imezuia mpango wa jimbo la Kerala Kusini mwa nchi hiyo kupiga marufuku pombe. Mamia ya wamiliki wa baa walikuwa wamepinga marufuku hiyo ambayo ingeanza kutekelezwa Ijumaa hii kwa kusema kuwa … Read More
  • Mahakama:Pistorius hakukusudia kuuaJaji anayetoa uamuzi katika kesi ya mauaji inayomkabili Oscar Pistorius, amesema upande wa mashitaka umekosa kuthibitishia kikamilifu shitaka kuu la kwanza dhidi ya Pistorius kuwa alikusudia kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp… Read More
  • Mchakato wa katiba kusitishwaKumekuwa na maoni tofauti kufuatia hatua ya kusitisha mchakato wa kura ya maoni ya Katiba Mpya nchini Tanzania. Katika kikao cha Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na Viongozi wa vyama vya siasa nchini humo wamekubaliana kuwa ku… Read More

0 comments:

Post a Comment