‘Beautiful Onyinye’ na kipenzi cha Diamond, Wema Sepetu sasa ni
mjamzito. Baada ya misukosuko ya muda mrefu ikiwemo kuporwa na
wasichana wenzake penzi lake la Diamond, sasa Wema amepata kile
alichokuwa akikililia kwa muda mrefu….
Chanzo cha habari hii kutoka kwa marafiki wa Diamond kimedai
kuwa Wema amenasa ujauzito na kugundulika hivyo walipokuwa
Afrika Kusini kwenye tuzo za MTV-MAMA na kumfanya Diamond
achanganyikiwe kwa furaha….
Kwa mujibu wa chanzo hicho, inadaiwa kuwa Diamond kwa sasa kawa
kama mtu aliyepagawa kwa furaha kutokana na taarifa hizo
njema na tayari ameshaanza maandalizi ya kijacho chake….
Kugundulika kwa ujauzito wa Wema ni baada ya kuanza kujisikia
vibaya walipokuwa Afrika Kusini ikiwemo kichefuchefu na
kizunguzungu alipokuwa hotelini alipofikia na kulazimika kwenda
hospitali kwa uchunguzi zaidi….
Inasemekana kuwa Wema alisindikizwa na Aunt Ezekiel kwenda
hospitalini waliyekuwa naye huko Afrika Kusini kumpa sapoti
Diamond na madaktari ndiyo waliomjuza kuwa anakiumbe tumboni
cha wiki 7
Taarifa za madaktari hao zilimfanya Wema awe kama mwehu
aliyepagawa na kurudi hotelini kwa mumewe Diamond huku akiwa
na tabasamu ambalo hapo awali Diamond hakuwahi kuliona….
Inasemekana kuwa mpaka sasa siyo Diamond wala Wema aliyewaambia
wazazi wake kuhusiana na mimba hiyo zaidi ya watu wa karibu
wa wawili hao waliowasindikiza Afrika Kusini.
Tumehamia
katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali
kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi
vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com
0 comments:
Post a Comment