Facebook

Thursday, 12 June 2014

Majambazi wafanya mauaji kituo cha Polisi Kimanzichana !

 


       TANZIA: Mnamo 11/06/14 majira ya saa 7 mchana huko kituo kidogo cha Kimanzichana Pwani, watu wasiojulikana waliojifanya kuwa ni raia wema waliingia kituo kidogo cha Polisi Kimanzichana huku wakikimbia wakiwa na silaha za jadi kiasi cha askari wa zamu kuamini kuwa ni watu wanaohitaji msaada. 

          Cha kushangaza watu hao walimvamia askari mwenye silaha ambaye amefahamika kwa jina la JOSEPH NGONYANI na kuanza kumkatakata mapanga na hatimaye kupora silaha SMG ikiwa na risasi 30. 
 
          Ndipo walipoanza kushambulia kwa risasi askari wengine na kufanikiwa kupora SMG ya pili na risasi 30. 
Hatimaye watu hao wakapora risasi za akiba 41 na kutoweka kusikojulikana. Askari Ngonyani alifariki dunia alipokuwa anapatiwa matibabu kwenye hospitali wilaya ya Mkuranga.
       
 Askari mwingine aitwaye VENANCE amejeruhiwa mgongoni kwa risasi ambayo bado imo ndani, na kwenye paja la mguu wa kulia. Mgambo Mariam alijeruhiwa kichwani, shingoni na kuvimba bega kutokana na kupigwa sana mateke na kujeruhiwa mbavuni.

   Kwa mujibu wa mganga Mkuu wa zamu wa Hospitali hiyo aitwaye VERONICA MUSIME, anathibitisha askari huyo kufariki akiwa anapatiwa matibabu hapo Mkuranga wakati wengine wamekimbizwa Muhimbili kwa matibabu ya kina.
           Kazi ya Mungu haina makosa; vituoni tuwe makini sana na stahili hii ya ujambazi; HESHIMA PEKEE kwa marehemu na majeruhi hawa ni kuwapata watuhumiwa wote na silaha walizoiba bila kuchelewa. Bila kujali mkoa ulipo, taarifa za haraka tunatarajia kupata toka kwako kuhusiana na wahusika wa tukio hili. AMEN
Tuko katika maboresho hivi karibuni blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma zetu za kutoa habari na burudani.Tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi.Vitu vizuri vipya usivyotarajia utaviona na kufurahia kupitia www.bantutz.com....

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment